MJASILIAMARI AWAITA WANANCHI KUPATA KEKI,MAPAMBO KUPITIA KAMPUNI YAKE
Na David John
WAJASIRIAMALI kote nchini wanapaswa kuchangamkia fursa za mikopo ya wajasiriamali inayotolewa Serikalini kwa lengo kujikwamua kiuchumi na kupata nafasi ya kuchangia uchumi wa nchi Kwa ujumla .
Mwito huo umetolewa septemba 29 kwenye maonyesho ya sita ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita na Cecylia Miraji mjasiriamali ambaye anajishughulisha na mapishi, vitafunwa keki ambaye pia mshindi wa tuzo ya mwanamke kinara wa mapishi lands ya ziwa .
Cecylia amesema kuwa uwepo wa mikopo hasa taasisi za kifedha zinasaidia wajasiriamali kujikwamua kiuchumi na kuendesha familia zao nakwamaba kupitia Nice Creative Cakes na vitafunwa wanawalika wananchi pia kuchangamkia fursa za kupata keki,Bora ,mapambo, na vitafunwa.
Pia amesema kuwa endapo mtu atakopa na akatumia kwa lengo husika ni rahisi kujeresha mikopo hiyo badala yakutumia tofauti na lengo husika.
kuhusu biashara ya upishi wa keki a
mbayo imemuwezesha kupata tuzo amesema kuwa kazi hiyo imemfanya kupiga hatua za kinaendelea ikiwemo kulea na kusomesha watoto huku akitaraji kufanya mambo makubwa kupitia biashara hiyo.
Amefafanua kuwa Yeye yupo Kanda ya ziwa katika Mkoa wa Geita ,mtaa wa bomani karibu kabisa na Kampuni ya GGMl.na Kwa mawasiliano yao 0767 093444.
"Hii biashara ya vitafunwa na keki inamuwezesha kujikwamua kiuchumi niwashauri wanawake wenzangu wasibweteke watafute walimu wajifunze upishi wa keki na vutafunwa wataendesha maisha waache uoga wakuthubutu"amesema secylia