TRA YAKUSANYA TRILION 6.63 YA ROBO YA TATU YA MWAKA WA FEDHA 2023/24

 




Na Mwandishi wetu 

MENEJIMENTI ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),imesema kuwa katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/24 imefanikiwa kukusanya kiasi cha sh. Trilioni 6.63,ikiwa ni sawa na asilimia 95.17 ya lengo la kukusanya sh.Trilioni 6.97.
 

Taarifa iliyotolewa jana na TRA kwa umma  na kusainiwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata juu ya Makusanyo ya Kodi katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/24,imesema  makusanyo hayo ni ongezeko la asilimia 11.68 ikilinganishwa na makusanyo ya sh.Trilioni 5.94 ya kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha 2022/23

Aidha amesema kwamba katika kipindi cha mwezi machi mwaka huu,TRA ilifanikiwa kukusanya kiasi cha sh.Trilioni 2.49 sawa na ufanisi  wa asilimia 97.05 katika lengo la kukusanya kiasi cha fedha sh. Trilioni 2.56 ambapo ni ongezeko la asilimia 6.91 ukilinganisha na kiasi ca sh.Trilioni 2.23 kilichokusanywa mwaka uliopita wa fedha.

Aidha akizungumzia mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/24 yamechangiwa na mambo mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa uhiari wa ulipaji kodi kufuatia maboresho yanayoendelea kufanywa kama kusogeza huduma jirani na walipakodi.

Akitaja mafanikio mengine ni kuwepo kwa muitikio mzuri wa walipakodi kuwasilisha kwa wakati ritani za kodi kwa mwaka 2024 kupitia mifumo ya teham,kuongezeka kwa miradi ya uwekezaji na ukuaji wa shughuli za kiuchumi nchini na kuongezeka kwa ufanisi kwenye huduma za forodha hususan katika kusimamia kodi.

Kamishna Kidata amesema katika kuhakikisha kuwa lengo la makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2023/24 inafanikiwa ni vema wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa TRA juu ya vitendo vinavyoashiria ukwepaji wa kodi nchini ikiwemo katika biashara za magendo.

''TRA inapenda kusisitiza kuwa wafanyabiashara wote wanashauriwa kuendelea kutoa risiti za kielektroniki (EFD)zenye viwango sahihi kila wanapouza bidhaa au kutoa huduma ,''amesema na kuongeza

''Menejimenti na bodi ya TRA inapenda kuwashukuru walipakodi na watanzania wote kwa kuendelea kutoa ushirikiano wa kulipa kodi na kuthamini juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongezwa na Rais Samia Suluhu Hassan,''amesema.

Powered by Blogger.