WACHIMBAJI CHANGAMKIE HISA SOKO LA MITAJI
Na Mwandishi wetu.
MKUU wa kitengo cha utafiti ,masoko na Maendeleo kutoka kampuni ya Orbit Securities limited Fortius W.M Rutabingwa Amesema orbit security ni kampuni ya wakala wa Soko la Hisa na wamekuja Kwa mara ya kwanza kwenye maonyesho ya kimataifa ya sita ya teknolojia ya madini yanayofanyika mkoani Geita Kila mwaka.
Amesema kuwa wao kama orbit wameshiriki kwa mara kwanza na malengo ni kuwaelimisha washiriki hasa wadau wa sekta ya madini juu ya fursa zilizopo kwenye soko la Hisa au mitaji ambapo kwenye upande wa uwekezaji kwenye hisa na upande wa hati fungani watu wanoshiriki sana kwenye biashara za madini wengi huwa wanapata pesa nyingi Kwa ghafla au Kwa mkupuo hivyo wanaonyeshwa ni fursa zipi ambazo wanaweza kuweka pesa zao na zikawa salaama.
Rutabingwa ameyasema haya Septemba 30 mwaka huu kwenye kilele cha maonyesho ya sita ya teknolojia ya madini ambayo yanafanyika mkoani Geita.
Rutabingwa Amefafanua kuwa kuweka pesa kwenye eneo la Hisa pesa zinakuwa salama huku wenyewe wakiendelea na shughuli za madini ,na mwitikio ulikuwa sio mkubwa sana Kutokana na maeneo hayo kutojua na kukosa ufahamu wa kutosha kuhusu fursa zilizopo kwenye soko la mitaji .
Amesema sehemu nyingine ambayo wao wamekuwa wakiisisitiza nikuhusu wa chimbaji wadogo au wa kati ambao wanandoto za kukuza mitaji yao na kwamba badala ya kutegemea kupata mitaji kwenye mabanki lakini pia nifursa zipo kwenye soko la mitaji
Pia amefafanua uwekezaji ukiwa kwenye soko la mitaji na kwenye migodi ya madini kunahitaji uwekezaji wa mtaji mkubwa na wamuda mrefu hivyo walikuja kuwaelimisha wananchi ili kutambua umuhimu wa hisa na hapa nimuhimu wananchi wakaungauna na hata kama mtu akiwa mmoja basi orbit wanaweza kukushika mkono .
Amesema kuwa kupitia maonyesho hayo wamefanikiwa kupata watu wachche na wamejaribu kuongea nao lakini kwasababu maarifa hayo kwao yalikuwa sio makubwa Sana ila mwitikio umeonekana na kwakweli huo ni Mwanzo na wanatakiwa kuendelea na kutembelea mtu mmoja mmoja na kwenye vikundi vyao vya uchimbbaji ili kutoa elimu.
Ameongeza kuwa Soko la mitaji Tanzania dhamira yake nikuona wanafadhiri kweli na likiwa na msaada mkubwa Kwa wachimbaji hasa Tanzania hivyo wanakwenda kujipanga kwani wameweza kujua umoja na vikundi vyao hivyo wanarudi ofisi ili kuweza kujipanga
Amesema mwaka huu ni wasita maonyesho yanafanyika lakini bado mchimbaji anajiita mchimbaji mdogo hivyo lazima wakuwe na kwenda kwenye mchimbaji wa kati na mkubwa na Kampuni ziliizokuwa binafsi basi ziwe kampuni za umma .
Ameongeza kuwa kupitia Soko la mitaji wananchi kama wanakuwa wameshajiunga na kuwa na sifa wao wataendelea kuwapa mitaji ya muda mrefu kwani tayari watakuwa wameshakuwa na uwazi kwenye shughuli zao .
Mwisho wanaishikuru Serikali Kwa kuweka sera na kufanya maonyesho hayo yanafanyika na kilichobaki nisekta binafsi Sasa kufanya kazi ili kuweza kufikia malengo nakwasasa wanapatikana Dar es Salaam katika posta mpya.