BALOZI DKT.BATILDA ATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI


Na Mwandishi wetu,Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi.Dkt.Batilda Burian amewatembelea majeruhi wa Ajali ya Basi iliyotokea Wilayani Nzega Mkoani Tabora ambao wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mji Nzega na Hospitali ya Rufaa Nkinga .

Baada ya kufika katika hospital hizo aliwafikishia salamu za pole  kutoka kwa Rais.Samia Suluhu Hassan na kuwapa posho ya kujikimu pamoja na Asali lita moja kila mmoja kwa matumizi ya Chakula na Tiba.

"Mpaka sasa kati ya majeruhi 60 waliobaki hospitali  ni 19 na wote wanaendelea vizuri. Wawili wapo Bugando nao wanaendelea vizuri. Miili kumi na tatu tayari imekwisha tambuliwa bado miili 5 ambayo tunaendelea kuwatafuta ndugu na jamaa zao, ikumbukwe kuwa basi la Alpha lilikuwa linatoka Mwanza siku hiyo ya tarehe 21 Oktoba,2023 kwenda Dar-es-Salaam.Tunaomba tufuatilie ndugu na jamaa zetu ili miili yote iweze kuchukuliwa na kusitiriwa". amesema na kuongeza 



"Tunaendelea kutoa pole kwa ndugu na jamaa wa wote waliofariki katika ajali hiyo mbaya" .ameawma Balozi.Dkt.Batilda Burian .



.

Powered by Blogger.