Bili 1 zatumika kuelimisha makuzi ya Albino nchini


Na Mwandishi wetu 

SHIRIKA  linalojishughulisha na kutoa huduma za kielimu na kiafya kwa watu wenye ualbino 

la Inside The Side lenye Makao Makuu yake Nchini Uholanzi  limeanza programu maalumu ya kutoa elimu kwa vijana nchini Ili kuwawezesha kukua wakijua malezi na makuzi ya watoto wenye ualbino

Akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika hilo Desiree Schoonen alisema, elimu hiyo itatolewa mashuleni na vyuoni kwa njia ya hadithi kupitia filamu iitwayo White Berry

Alimtaja mhusika Mkuu kwenye filamu hiyo kuwa ni  Latifa Mwazi  ambaye naye pia alizaliwa akiwa albino mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

" Filamu hii itakuwa ni mahususi kwa ajili ya kuelimisha Jamii kuhusu malezi na makuzi ya watu wenye ualbino  na tumeanzia mashuleni na vyuoni Ili kundi rika hili liweze kukua na kutambua kuwa kila binadamu ana haki za msingi ikiwa ni pamoja na kuishi,' alisema Schoonen na kuongeza kuwa elimu hii ni mwanzo lakini lengo ni kufikia nchi nzima

Alizitaja baadhi ya shule na vyuo ambavyo vitafijiwa na elimu hiyo katika awamu ya kwanza kuwa ni pamoja na shule ya msingi St Anne Maria ya Mbezi  Jijini Dar es Salaam, Chuo Cha UDOM,KCMC Moshi na IAA  Cha Arusha

Schoonen aliushukuru ubalozi wa  Uholanzi nchini Tanzania kwa kufadhili.kila hatua ambayo imefanikisha kukamilika kwa filamu hiyo ambapo mpaka kukamilika kwake zaidi ya Sh. Bilioni 1 zimetumika

Kwa upande wake mhusika  Mkuu kwenye filamu hiyo Latifa  Mwazi alisema kutokana na Jamii kunyanyapaa watu wenye ualbino ameamua kuwa balozi kwa kuandaa filamu hii Ili ielewe kuwa ualbino siyo umasikini badala yake ni binadamu kama wengine na anaweza kufikia.mbali kiuchumi

Amewataka wazazi na walezi kuacha kuwafungia ndani watoto wenye ualbino badala yake wawapeleke shule Ili kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Amewaongeza kuwa kutokana na elimu aliyoipata kuhusu haki  za albino hajutii kuzaliwa albino kwani mpaka.sasa anaishi maisha mazuri na tayari amekuwa raia wa Uholanzi

"Mwanzo ulikuwa mgumu sana kwangu nilijijatia tamaa nikawa najiina wa tofauti lakini sasanimetambua albino ni binadamu kama wengine na akipatiwa haki zote za msingi kama.binadamu wengine anaweza kufika mbaki kiuchumi na hata kwenye uongozi," alisema Mwanzi

Aliongeza kuwa filamu hii kwa Sasa imeanza kuoneshwa mashuleni na vyuoni lakini mapema  mwakani itaanza kuoneshwa kwenye Mabasi ya mikoani Ili kila mtu akiwa safarini  aweze kupata elimu hii

" Filamu hii kwa Sasa inaoneshwa kwa lugha ya kigeni lakini hadi kufikia.mwakani itakuwa imetafsiriwa kwa lugha ya taifa Ili kila.Mtanzania aweze kuelewa kinachosimuliwa na kuwa balozi kwa mwingine

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Mabasi Tanzania ( UWAMATA) Majura Kafumu aliushukuru uongozi wa Shirika la Inside The Side kwa kuona umuhimu wa filamu hii kuoneshwa ndani ya Mabasi ya mikoani kwani kufanya hivyo Jamii kubwa itaelimika 

" Kuoneshwa kwa filamu hii ndani ya Mabasi yaendayo mikoani  kutasaidia kuelimisha  janiii kutambua kuwa watu wenye ualbino ni ndugu zetu, na  wana haki kama binadamu wengine na wanaweza kufika mbali endapo wakipatiwa malezi bora kutoka kwa wazazi, walezi na Jamii

Pia alisisitiza kuiasa Jamii kuacha tabia za kuhusisha kundi hili na Imani za  kishirikina kwani kufanya hivyo ni kosa ambalo linaweza kusababisha kupoteza haki zao za kimsingi ikiwepo elimu na afya

Hata hivyo alisema.elimu hiyo kwa vijana ambao ni kundi rika itawezesha kutengeneza kizazi bora chenye  kupinga unyanyapaa dhidi ya watu wenye ualbino


Powered by Blogger.