TBA KUWACHUKULIA HATUA WADAIWA SUGU WA KODI YA PANGO

 



Na Mwandishi wetu

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) imesema hadi kufikia Octoba 31 mwaka huu inadai zaidi ya Billioni 7.8 za Kodi ya pango kutoka kwa wapangaji wa nyumba huku Billioni 3.5 ni madeni ya Taasisi mbalimbali za Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo Novemba 22 mwaka huu Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch Daud Kondoro amesema moja ya hatua TBA itakazochukua ni pamoja na kuwaondoa wadaiwa sugu kwa nguvu kupitia dalali wa mahakama Wins Auction Mart

Amesema kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya wapangaji wa nyumba za TBA kutolipa kodi ya pango kwa wakati hali inayosababisha kuwa na malimbikizo makubwa ya madeni huku baadhi wakiamini nyumba hizo ni mali ya umma hivyo hawawezi kutolewa.

Akitaja mikoa inayoongoza kwa madeni hayo ni pamoja na Dodoma, Arusha,Mwanza na Mbeya ambapo deni kubwa la kodi ya pango la sh. bilioni 1.4.

Arch Kondoro amesema tayari kampuni ya udalali wa mahakama iitwayo Wins Auction Mart imeshakabidhiwa orodha ya wadaiwa wote kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa na hatua hiyo itaanza Desemba Mosi, mwaka huu, kwa nchi nzima.

Powered by Blogger.