FCS YATARAJIA KUONA MABADILIKO YA KISHERIA ,SERA NA UTEKELEZAJI

 


Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam

SHIRIKA lisilokuwa la Kiserikali la F huuoundation for Civil Society(FCS) limesema linatarajia kuona mabadiliko ya kisheria sera na utekelezaji wa sehemu ya sheria ili Asasi za kiraia ziweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.


Mabadiliko hayo yanaonekana kubadilika kupitia mradi wake wa "Uraia wetu"ambao unalenga kuangalia mazingira wezeshi ya Asasi za kiraia katika kutekeleza majukumu yake pamoja na kushirikiana na Serikali.

Akizungumza na Waandishi wa habari  Jijini Dar es salaam 

Mratibu wa Miradi kutoka FCS,Nicholas Lekule  katika hafla ya kufanya tathimini ya mradi huo,amesema  mradi huo wa uraia wetu ulianza Julai  mwaka huu na  unatekelezwa kwa miaka mitatu Tanzania bara na Visiwani .

Amesema mradi huo unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa FCS ilitoa ruzuku kwa wadau 15 ambao wamefanya kazi katika maeneo tofauti.


"Tumekutana kufanya tathimini ya mdau mmoja wapo ambaye alifanya kazi katika nyanda kusaini ili tuangalie ni kwa namna gani amefanikiwa katika mradi huo wa Uraia wetu "alisema na kuongeza kuwa 

"Lengo zaidi ya mradi huu ni kuzijengea uwezo Asasi ziweze kufanya shughuli ambazo zitasaidia kuleta mabadiliko"amesema Lukule


Vilevile amesema malengo FCS ni kuona baada ya miaka mitatu  Asasi za kiraia zinaratibiwa vizuri na kufanya kazi Kwa ufanisi zaidi .

Akizungumzia kuhusu vigezo vilivyochukuliwa kwa asasi hizo  amesema waliangalia suala la uwakilishi na wadau wenye uzoefu katika maeneo husika.

Aidha amesema  mradi huo utanufaisha Taasisi nyingine sio tu hizo 15 ili mwisho wa siku sekta ya Asasi za kiraia iweze kuimarika zaidi na mazingira ya ufanyaji kazi bora.


Kwa upande wake Mkurungenzi wa Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mtwara  (MTWANGONET) Fidea Ruanda ambaye ni mmoja ya Asasi zilizopewa ruzuku ya utekelezaji wa mradi huo amesema mradi huo umefadhiliwa na FCS ulianzwa kutekelezwa Julai 2023 na utatekelezwa Kwa miaka mitatu.

"Mradi huu ulilenga kuangalia mazingira wezeshi ya Asasi za kiraia katika kutekeleza majukumu yake pamoja na kushirikiana na Serikali"amesema Ruanda

Amesema MTWANGONET imetekeleza mradi huo katika mikoa Saba ambayo ni mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe pamoja  Rukwa. No

Akitaja chagamoto alizokutana nazo katika mradi huo ni kuwepo kwa uelewa mdogo kuhusu sera, sheria na miongozo.

Aidha amesema  bado ushiriki wa wadau ni mdogo hivyo alisisitiza ni muhimu kuwa na umoja Ili kuweza kusukuma ajenda mbalimbali.

Powered by Blogger.