AWESO AFANYA ZIARA YA KIKAZI CHANZO CHA MAJI IHELELE



 Na Mwandishi wetu

Waziri wa Maji,Jumaa Aweso amefanya ziara ya kikazi kwenye chanzo cha maji cha Ihelele, wilanyani Misungwi mkoa wa Mwanza kinachosimamiwa na kuendeleshwa na mamlaka ya KASHWASA 

Chanzo cha Iherere  ni chanzo pekee cha Skimu ya maji kutoka ziwa Victoria inayohudumia mikoa sita ikiwa ni pamoja na Shinyanga, Mwanza,Geita,Simiyu,Tabora na Singida.

Aidha chanzo hiki kinapeleka maji katika  Mamlaka za Maji nane(8) ambazo ni SHUWASA,KUWASA,MAGAWASA,KIWASA,TUWASA,NZUWASA, IGUWASA na MWAUWSA-NGUDU. Vilevile Vyombo wa Watoa huduma ya maji safi ngazi ya jamii( CBWSO )  zipatazo 95 na Migodi 3,inapata  huduma ya maji kupitia Skimu hii.



Powered by Blogger.