MWENYEKITI WA ACT -WAZALENDO DODOMA ASIMAMISHWA UONGOZI

 



Na Mwandishi wetu,Dodoma 

Chama cha ACT Wazalendo kinafuatilia kwa karibu mwenendo wa mambo katika mjadala wa kitaifa unaoendelea kuhusu Miswada ya Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Ikumbukwe kuwa msimamo wa ACT hi Wazalendo ambao unatokana na azimio la Kamati Kuu ya ACT Wazalendo iliyokutana tarehe 20 Desemba, 2023 ni kuwa miswada hiyo ina mapungufu kwa sababu haijaakisi maoni ya wadau yaliyotolewa kwenye majukwaa mbalimbali.

Chama chetu kilitoa rai kwa Serikali na Bunge kuhakikisha kuwa miswada hiyo inafanyiwa maboresho makubwa hasa kwa kujumuisha masuala ambayo tayari yalipata muafaka wa kitaifa na kukubalika na wadau wengi. Jopo la viongozi wa Chama chetu likiongozwa na Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe liliwasilisha maoni yake mbele ya Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria. Ni imani yetu kuwa maoni hayo ambayo kwa hakika ndio maoni ya wadau wengi, yatazingatiwa.



Kamati Kuu ya Chama chetu itakutana tarehe 27 Januari, 2024 kwenye kikao chake cha kawaida. Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu itafanya tathmini juu ya hali ya kisiasa nchini ikiwemo kuangazia mwenendo wa mambo ndani na nje ya Bunge kuhusu mjadala wa miswada hiyo.




Katika hatua nyingine, tunapenda kuujulisha umma kuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Dodoma Ndugu Yohana Mussa ambaye alitoa kauli kwa vyombo vya habari zinazokinzana na msimamo wa Chama chetu kwenye miswada hiyo mitatu amesimamishwa uongozi na kutakiwa kujieleza. Suala lake litapelekwa kwenye kikao kijacho cha Kamati Kuu kwa ajili ya maamuzi.

Powered by Blogger.