RAIS DKT.MWINYI AKUTANA NA MWENEZI MAKONDA IKULU ZANZIBAR

 


Na Mwandishi wetu, Zanzibar 

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa Paul  Makonda, Ikulu Zanzibar tarehe: 11 Januari 2024.

Aidha Katibu Mwenezi Makonda amempongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kazi nzuri anayoendelea kufanya kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 kipindi cha Miaka 3 kwa miradi mbalimbali ya maendeleo Zanzibar. 

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi  ampongeza Katibu Mwenezi Makonda kwa kuteuliwa kwake na kuanza kazi vizuri  ya ujenzi wa Chama cha Mapinduzi kwa umma.


Powered by Blogger.