SERIKALI :MAANDALIZI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KUPAMBA MOTO


 Na Mwandishi wetu,Dar

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohammed Mchengerwa,amesema Serikali imejiandaa vizuri katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba ,mwaka huu kwa kutumia fedha zake za ndani na sio kuomba kwa watu.

Amesema kwasasa wanaendelea na kalenda ya mapitio ya kanuni na maandalizi mengine ambayo yametimia kwa asilimia kubwa kufanyika kwa uchaguzi huo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari, Mchengerwa amesema uchaguzi huo wa serikali ya mitaa upo kwa mujibu wa kalenda hivyo wakati ukifika taarifa zitaweza kutolewa kwa usahihi.

Amesema serikali imejiandaa vizuri kwa sababu inafedha za kutosha kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika.''Serikali itatoa fedha yenyewe na maandalizi yapo vizuri tupo katika hatua nzuri tutakapofika hatua ya kutangaza tarehe tutawafahamisha kwani ni kalenda ya mwaka mzima,''alisema na kuongeza

''Kalenda hiyo imeanza kuanzia Oktoba 2023  na itaenda hadi Novemba mwaka huu ambapo ndipo tutakapo hitimisha viongozi waliopo madarakani wa serikali za mitaa,''amesema.
Powered by Blogger.