TANZANIA KUWA MWENYEJI MKUTANO WA 10 WA JOTOARDHI

 



Na Mwandishi wetu 

NCHI ya Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa kongamano la 10 la  Jotoardhi ambapo takribani washiriki 1000 kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kushiriki .

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam leo Machi 18 na Kamishna wa Umeme na Nishati yadilifu kutoka Wizara ya Nishati ,mhandisi Innocent Luoga wakati akifungua mkutano wa maandalizi ya kongamano hilo.

Amesema kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Novemba 11 hadi 17 mwaka huu  ambapo nchi 50 zinatarajiwa kushiriki.

"Kongamano hili uendelezaji wa jotoardhi katika nchi za ukanda wa Mashariki ya Afrika ambapo katika nchi hizo zipo nchi sita wanachama katika ukanda ambazo ni pamoja na Tanzania, Kenya , Uganda, Ethiopia, Rwanda, jibuti."amesema mhandisi Luoga.

Amesema washiriki wa kongamano hilo ni wataalamu wa jotoardhi pamoja na wafadhiri wa miradi, na sekta binafsi za kuendeleza miradi mbalimbali.

"Nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano huu ni baada ya mwaka 2022 Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kukubali ombi la Shirika la kimataifa la mazingira la Tanzania kuwa mwenyeji wa kongamano hilo ambalo ufanyika kila baada ya miaka miwili katika nchi mwanachama"amesema mhandisi Luoga 

Akitaja faida za kongamano hilo  kufanyika hapa nchini mhandisi Luoga amesema ni pamoja na kupata manufaa mbalimbali ikiwemo kuharakisha utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa.

Sambamba na kuasaidia kubadilishana uzoefu na utaalamu mbalimbali katika   utekelezaji wa miradi mbalimbali 

Aidha amesema nchi ya Tanzania ina rasilimali ya jotoardhi ambayo inaweza kuzalisha megawati za umeme 5000.

Mhandisi Luoga ameeleza kuwa sera ya nishati inataka uzalishwe umeme kwa kutumia vyanzo mchaganyiko ili kuwa na umeme wa uhakika.

"Sasa tunataka kuzalisha umeme kwa kutumia jotoardhi tunatambua nchi yetu kwa Sasa inazalisha Umeme Kwa kutumia maji, bwawa la mwalimu Nyerere, gesi pamoja jua."amesema

Amesisitiza kuwa Tanzania kuwa mwenyeji nwa kongamano hilo ni Moja ya mikakati ya kuhakikisha inakuwa na umeme wa uhakika na salama katika nchi bila ya kuathiri shughuli za kijamii na kiuchumi.

Aidha amesema kongamano Hilo pia litaweza kuleta makubwa ikiwemo kuitangaza TGDC pamoja na kukaribisha wafadhiri  Kwa ajili ya kufanya tafiti.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya uendelezaji jotoardhi Tanzania (TGDC) Mhandisi Mathew Mwangomba  aliiushukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wanasonga mbele katika kuhakikisha wanakuwa na nishati yadilifu ya jotoardhi.

Amesema lengo la mkutano huo ni kuharakisha maendeleo ya rasilimali jotoardhi Tanzania pamoja na kuangalia masoko ya gesi ya ukaa .

Vilevile amesema mbali na kuharakisha maendeleo pia kongamano hilo litawakutanisha  wadau wa ndani na nje kwa ajili ya kuhakikisha kupata nishati ya jotoardhi Tanzania. 


"Uwepo wa jotoardhi Tanzania na kongamano hili nchini Tanzania wataalamu watu ndani pamoja na sekta zinazofugamana ikiwemo vyuo vikuu, kilimo, utalii tutaweza kukutana nao hii itasaidia kuharakisha upatikanaji wa jotoardhi Tanzania "amesema mhandisi 

"Sisi kama TGDC ni tunahakikisha nishati ya jotoardhi inasonga mbele katika upatikanaji wake .. upatikanaji wake unaendana na hatua tatu ambazo ni pamoja na kuwa na sayansi ya derojia , joto fizikia , joto kemia "amesema


Powered by Blogger.