UELEWA KUHUSU USONJI WAONGEZEKA



Na Mwandishi wetu

KATIKA kuadhimisha siku ya Usonji  Duniani kila ifikapo Aprili 2  kila mwaka uelewa katika jamii  umetajwa kuongeza kutokana kuwepo kwa elimu ya kutosha tofauti na miaka ya nyuma.

Hayo yamebainishwa  Jijini Dar es salaam leo Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Lukiza Autism foundation  wakati alipotembelea Shule ya Msingi ya Msimbazi Mseto kitengo cha watoto wenye usonji kwa ajili ya kujumuika nao pamoja .

Amesema kwa sasa jamii inauelewa wa kutosha tofauti  na miaka ya nyuma kwani  wazazi na walezi weweza kuelewa na kuwatambua mapema watoto hao.

"Licha uelewa kuongezeka ..bado vijijini elimu ni ndogo kutokana na baadhi ya watu kuhusisha na Usonji na imani za kishirikina hivyo  bado tunaendeleza elimu"amesema Hilda

Aidha amesema kukubalika katika jamii kumeanza kuonekana kwa kiasi jambo ambalo limesaidia kupunguza   kuchekwa, kuziaki na kubezwa.

Vilevile amesema ipo haja ya kuwa na kituo ujumuishi ambao utasaidia kupatikana Kwa elimu sehemu yoyote ili kuondoa chagamoto watoto wanaoishi au kutoka mbali.

Mkurugenzi huyo ambaye nae ni mama wa mtoto wenye Usonji alisema  ulezi wa watoto wenye usonji sio wa mtu mmoja bali ni wajamii nzima.

"Mimi nilijua chagamoto ya mtoto wangu mapema tangu akiwa na miaka miwili na nusu hii ilinisaidia kumjua mtoto mapema na kuweza kumsaidia pia ilinipa mda wa kukubali hali yake "amesema Hilda

Aidha amesema Serikali imeweza kusikia kilio cha watoto wenye usonji ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika elimu na mazoezi tiba.

"Tunamshukuru Serikali Kwa kuendelea tuunga mkono ila tuniomba iweze kuongeza shule kwa ajili ya watoto wenye usonji pamoja dawa"amesema

Pia amesema licha ya kuwepo jwa uelewa katika jamii ni muhimu kuanza kufanyika kwa tafiti juu ya chanzo Cha ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuanza kulifanyia kazi dhana zinazotajwa.

Kwa upande wake Daktari kutoka Taasisi ya AfyaCheck ambao ni wasimamizi huduma kwa watoto wenye usonji waliopo shule mbalimbali ikiwemo Msimbazi Mseto Isaac Maro amesema usonji ni Hali ambayo utokea Kwa mtoto na kuishi maisha yake yote .

"Hali hii uwa na viashiria vikuu vitatu ikiwemo mawasiliano, ushidwaji wa kuchagamana vizuri pamoja na kuwa na tabia za kujirudiarudia hivi ndivyi viashiria vikuu vinavyoonekana kwa watu wenye usonji"amesema.

Amesema Hali hiyo kuonekana kwa watoto kuanzia miezi sita mpaka miezi 18 huku ikitegemewa ukaribu wa mtoto na mzazi

Naye mzazi wa mtoto mwenye usonji amesema Mecktrida Mtaki aliipogeza Taasisi ya Lukiza Autism foundation kwa kuwaunganisha na watoto wengine kujifunza mambo

Aidha amewaomba wazazi na walezi wenye chagamoto  ya usonji kutokuwafungia na badala yake amkutanishe na watoto wengine kwani anaweza kubadilika kupitia watoto hao.


Powered by Blogger.