SMZ INATHAMINI MCHANGO WA CRDB KATIKA KUKUZA UCHUMI-DK.MWINYI

 

Na Mwandishi wetu,Arusha 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ,Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inathamini sana mchango wa Benki ya CRDB katika kukuza uchumi  wa Zanzibar na kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar

Pia ameeleza kuwa CRDB imechangia kuendeleza sekta mbalimbali zikiwemo utalii, kilimo, elimu, michezo, ufugaji, uvuvi , biashara na ujasiriamali. 

Rais Dk.Mwinyi aliyasema hayo alipofungua semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB katika Ukumbi wa Kimataifa wa  Mikutano Arusha  (AICC) tarehe: 17 Mei 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema matarajio yake ni kuona taasisi nyingi za umma kutoka Zanzibar zinawekeza katika benki ya CRDB  ili kuendelea kuipa nguvu zaidi kuwezesha ushiriki wake katika miradi ya maendeleo.

Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  ikiwa mmoja wa wanahisa wa CRDB kupitia Mfumo wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), inajivunia sana utendaji wa CRDB. 

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi awapongeza Benki ya  CRDB kwa  mafanikio waliyopata katika mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa mkakati mpya wa biashara.

 Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa wanahisa kutumia vyema fursa ya kujifunza kupitia semina hii .

Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema  CRDB itakuwa mdau muhimu wa maendeleo ya Zanzibar na kuendelea kutoa ushirikiano.

Powered by Blogger.