BILIONI 2.9 KUJENGA CHUO CHA AFYA VWAWA MKOANI SONGWE

 


Na WAF - Dodoma

Ujenzi wa chuo cha Afya Vwawa Mkoani Songwe utaanza Oktoba, 2024 ambapo kwa sasa Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga jumla ya Tsh: Bilioni 2.9 kwa mwaka wa fedha 2024/25 kupitia fedha za mradi wa Mama na mtoto kwa ajili ya kujenga jengo mseto (Academic complex). 

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hayo leo Juni 11, 2024 katika Bunge la 12 mkutano wa 15, kikao cha 45 Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga aliyetaka kujua lini Serikali itajenga Chuo cha Afya Vwawa. 

Aidha, Waziri Ummy amesema tayari utaratibu wa kupata eneo umefanyika ambapo kiasi cha shilingi Milioni 151 kimetumika kwa ajili ya kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi waliopisha eneo hilo.


mesema, chuo hicho kitakua kinatoa mafunzo kwa ngazi ya Astashahada (Certificate) na Stahashada (Diploma) kwa kozi za uuguzi pamoja na kozi nyingine ambazo ni muhimu katika utoaji wa huduma za Afya ikiwemo wataalam wa maabara.

Powered by Blogger.