GSM TAYARI KUJENGA UWANJA YANGA
"Leo tupo na Mheshimiwa Mchengerwa(Mohamed- Waziri wa nchi, ofisi ya Rais TAMISEMI),
na tayari amepokea maombi yetu kuhusu mchakato wetu wa ujenzi wa Uwanja wetu hapa Jangwani. Jambo la kheri ni kuwa amejumuika nasi moja kwa moja akitokea Tabora. Mradi wetu huu wa ujenzi wa Uwanja tayari upo ofisini kwake na analifanyia kazi.
Mdhamini na mfadhili wetu GSM yupo tayari kutekeleza mradi wa ujenzi wa uwanja. Kwa bahati mbaya, GSM hajawahi kutoa ahadi hewa. Hivyo niwaahidi wanachama na mashabiki wetu kuwa mchakato wetu upo tayari kuanza kwa kuzingatia mradi wa mto Msimbazi" Injinia Hersi Said.
Naye Mhe. Mchengerwa aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo alisema;
"Rais Samia ameagiza zaidi bilion 400 zielekezwe kwenye mradi wa bonde la msimbazi. Mradi huo utaisaida sana kwenye malengo ya ujenzi wa Uwanja wa Yanga. Katika eneo hilo litajengwa daraja bora na la kisasa. Mchakato wa mradi huo utaanza mara moja na mradi wa Yanga utakuwa sehemu ya mradi huo.
Nimemwagiza mtendaji mkuu anayehusika na kuendeleza mradi wa mto msimbazi aonane mara moja na maofisa wa Yanga kukamilisha mchakato."