MPINA AKALIA KUTI KAVU BUNGENI
Spika wa Bunge Dk. Tulia Akson amelekeza Mbunge wa Jimbo la Kisesa(CCM), Luhaga Mpina afikishwe kwenye kamati ya maadili kwa kitendo chake cha kuupeleka ushahidi aliouwasilisha mbele ya waandishi wa habari kufuatia tuhuma dhidi ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwa madai kuwa alilidanganya Bunge.
Spika ametoa maelekezo hayo leo 18Juni 2024 Bungeni Dodoma ambapo amenukuliwa akisema;
"Naelekeza ifuatavyo, Kamati ya Haki, Maadili na madaraka ya Bunge ikutane mara moja kutafakari jambo hili lililofanywa na mhe.Mpina na kutoa maoni na mapendekezo ya nini kifanywe na Bunge"
Spika pia ameikabidhi Kamati hiyo ushahidi uliowasilishwa kwake na Mpina ili iuchambue na kulishauri Bunge huku vilivile akiitaka kuanza kazi mara moja leo 18Juni hadi Jumatatu Juni 24, 2924 itakapotakiwa kumkabidhi mapendekezo yake.