SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI-DK.MWINYI
Na Mwandishi wetu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imeendelea kuboresha mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji Zanzibar kwa kuboresha viwanja vya ndege ikiwemo ujenzi wa Terminal 2, ukarabati wa Terminal 1 na mpango wa ujenzi wa Terminal 4 katika uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Abeid Amani Karume na ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pemba .
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipozindua jina la brand ya Hoteli ya The Mora Zanzibar Matemwe, Wilaya ya Kaskazini B Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 12 Juni 2024.
Aidha Rais Dk.Mwinyi ameipongeza kampuni ya Tui Group kwa kuwekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 500 Zanzibar katika miradi ya hoteli mbalimbali zikiwemo hoteli ya Rui, Tui blue na The Mora Zanzibar.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa wawekezaji wa hoteli kuanzisha mfumo wa kidijitali wa kuonyesha mapato ya wateja wake katika kuisaidia Serikali kukusanya mapato stahiki, ameipongeza The Mora Zanzibar kwa kuwa mfano wa kuanzisha mfumo huo.