SIMBA HAKUJAPOA

 Anaandika Dr.Hamiss Kigwangalla, mwanachama mwandamizi wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam katika ukurasa wake wa mtandao wa X.

"GN 442 ya tar. 27/20/2017. Pitieni hii mnaopenda kujua transformation(Mabadiliko) ya Simba SC ilikwamia wapi. Mjue pia kwamba, mchakato wa kule FCC (Tume ya Ushindani) ulitoa maelekezo kadhaa ambayo hayakufuatwa. Hivyo mwekezaji wa Simba hana mamlaka yoyote yale ya kufanya anachokifanya, zaidi zaidi ni ubabe na uhuni tu.

Kwa kuwa watu wengi siyo weledi na hatuna muda wa kufuatilia mambo tunajikuta tunaburuzwa tu.

Mmoja anamwambia mwenzake jiuzulu, anajiuzulu. Wakati wa kujiuzulu anamteua mwenzake, kisha mwenzake naye anakubali uteuzi. Naye wakati wa kukubali uteuzi anamteua tena mwenzake.

Sikilizeni nawaambia: Kutokana na kelele hizi, kama serikali isipoingilia kati, wataweka mambo ya uwanjani sawa, wanasimba tutatulia. Hatutokuwa tumetibu tatizo, keshokutwa litaturudia tena. Mtakuja kunikumbuka tena. Amini nawaambia!

Tiba ya Tatizo ni Mfumo mbovu. Kuutibu ni kurekebisha, siyo hizi quick fixes na janja janja zinazofanywa. Hizi ni sawa na cosmetics tu! Uzuri wake haudumu.

Wanasimba lazima tujue kwamba:

1. Simba Sports Club Co. Ltd siyo kampuni halali - hivyo Bodi siyo halali. Hizo sarakasi zote zinazoendelea ni ubabe na uhuni tupu.

2. Thamani ya Simba ya miaka 8 iliyopita imepitwa na wakati. Haifai kutumika tena leo hii. Kuendelea na mchakato wa transformation kwa kutumia thamani ya zamani ya Simba siyo sahihi.

3. Mfumo wa utawala lazima uboreshwe tukitaka mafanikio tuliyoyatarajia wakati tunaanzisha mchakato huu. Muundo wa Bodi ya kampuni ya Simba Sports Club Co. Ltd ni lazima uboreshwe kuondoa janja janja na kutoa haki kwa wanahisa wenye shares nyingi zaidi, ambao ndiyo wenye timu yao (majority shareholders) na kuongeza uwazi zaidi kwenye muundo wa utawala. Yafuatayo yanaweza kufikiriwa:

(a.) Wawekezaji watakaonunua hisa lazima wasipungue watatu na wasizidi watano.

(b.) Mwenyekiti wa wanachama awe ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa SSC Co. Ltd sababu ndiyo ‘majority shareholders’!

(c.) Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa SSC Co. Ltd kama ni tisa basi watano watokane na uchaguzi wa wanachama wote na wanne wateuliwe na wawekezaji. Tena wawekezaji wapeleke majina matatu kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama ili mmoja kati ya hao achaguliwe kuwa mjumbe anayewakilisha mwekezaji aliyempendekeza.

(d.) Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi atachaguliwa na wanachama wote kutokana na majina matatu kupendekezwa na wawekezaji.

(e.) Wawekezaji watapendekeza majina ya CEO, CFO na COO. Watakopendekezwa watapaswa kuthibitishwa na Bodi kwa kura. Na Wataajiriwa na Bodi ya wakurugenzi ya SSC Co. Ltd na watawajibika moja kwa moja kwenye Bodi.

GN 442 ya tar. 27/20/2017. Pitieni hii mnaopenda kujua transformation ya @SimbaSCTanzania ilikwamia wapi. Mjue pia kwamba, mchakato wa kule FCC ulitoa maelekezo kadhaa ambayo hayakufuatwa. Hivyo mwekezaji wa Simba hana mamlaka yoyote yale ya kufanya anachokifanya, zaidi zaidi ni ubabe na uhuni tu.

Kwa kuwa watu wengi siyo weledi na hatuna muda wa kufuatilia mambo tunajikuta tunaburuzwa tu.

Mmoja anamwambia mwenzake jiuzulu, anajiuzulu. Wakati wa kujiuzulu anamteua mwenzake, kisha mwenzake naye anakubali uteuzi. Naye wakati wa kukubali uteuzi anamteua tena mwenzake.

Sikilizeni nawaambia: Kutokana na kelele hizi, kama serikali isipoingilia kati, wataweka mambo ya uwanjani sawa, wanasimba tutatulia. Hatutokuwa tumetibu tatizo, keshokutwa litaturudia tena. Mtakuja kunikumbuka tena. Amini nawaambia!

Tiba ya Tatizo ni Mfumo mbovu. Kuutibu ni kurekebisha, siyo hizi quick fixes na janja janja zinazofanywa. Hizi ni sawa na cosmetics tu! Uzuri wake haudumu.

Wanasimba lazima tujue kwamba:

1. Simba Sports Club Co. Ltd siyo kampuni halali - hivyo Bodi siyo halali. Hizo sarakasi zote zinazoendelea ni ubabe na uhuni tupu.

2. Thamani ya Simba ya miaka 8 iliyopita imepitwa na wakati. Haifai kutumika tena leo hii. Kuendelea na mchakato wa transformation kwa kutumia thamani ya zamani ya Simba siyo sahihi.

3. Mfumo wa utawala lazima uboreshwe tukitaka mafanikio tuliyoyatarajia wakati tunaanzisha mchakato huu. Muundo wa Bodi ya kampuni ya Simba Sports Club Co. Ltd ni lazima uboreshwe kuondoa janja janja na kutoa haki kwa wanahisa wenye shares nyingi zaidi, ambao ndiyo wenye timu yao (majority shareholders) na kuongeza uwazi zaidi kwenye muundo wa utawala. Yafuatayo yanaweza kufikiriwa:

(a.) Wawekezaji watakaonunua hisa lazima wasipungue watatu na wasizidi watano.

(b.) Mwenyekiti wa wanachama awe ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa SSC Co. Ltd sababu ndiyo ‘majority shareholders’!

(c.) Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa SSC Co. Ltd kama ni tisa basi watano watokane na uchaguzi wa wanachama wote na wanne wateuliwe na wawekezaji. Tena wawekezaji wapeleke majina matatu kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama ili mmoja kati ya hao achaguliwe kuwa mjumbe anayewakilisha mwekezaji aliyempendekeza.

(d.) Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi atachaguliwa na wanachama wote kutokana na majina matatu kupendekezwa na wawekezaji.

(e.) Wawekezaji watapendekeza majina ya CEO, CFO na COO. Watakopendekezwa watapaswa kuthibitishwa na Bodi kwa kura. Na Wataajiriwa na Bodi ya wakurugenzi ya SSC Co. Ltd na watawajibika moja kwa moja kwenye Bodi."

Powered by Blogger.