TPA YASAINI MKATABA WA MIAKA 30 NA KAMPUNI YA ADANI INTERNATIONAL
UCHUMI: Adani International Ports Holdings Pvt Ltd (AIPH) ambayo ni Kampuni tanzu ya Adani Ports and Special Economic Zone (APSEZ) imesaini Mkataba wa makubaliano wa Miaka 30 na Mamlaka ya Bandari Tanzania kuendesha na kusimamia Kituo cha Makontena cha 2 katika Bandari ya Dar es Salaam
Taarifa ya #APSEZ imesema Bandari ya Dar es Salaam ni bandari muhimu yenye Mtandao Mzuri wa Barabara na reli
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kituo hicho chenye gati nne, kina uwezo wa kushusha na kupakia mizigo ya Tani Milioni 1 kwa mwaka, ambapo kwa Mwaka 2023 kilisimamia tani Milioni 0.82 za makontena, takriban asilimia 83 ya jumla ya mizigo ya makontena ya #Tanzania