TRY AGAIN AREJESHWA SIMBA
Mwekezaji na Rais wa heshima wa Klabu ya soka ya Simba ya Dar es Salaam Mohamed Dewji- MO amefanya uteuzi wa wajumbe wapya wa bodi ya wakurugenzi huku zaidi ya nusu ya waliojizulu akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa bodi hiyo Salim Abdalah -Try Again wakirejeshwa.
MO amesema, "Kwa mamlaka niliyopewa kulingana na Mkataba wa Makubaliano na Simba Sports Club Limited (Memorandum of Association) na Kanuni za Makubaliano (Articles of Association), ibara ya 40; ningependa kuwatambulisha wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi kwa upande wa Mwekezaji."
Amewataja wajumbe hao kuwa ni Salim Abdalah-Try Again, Hussein Kita na Zulfikar Chandu.
Wengine ni Rashidi Shangazi, Mohamed Nassoro na Crecentius Magori huku wajumbe wa zamani, Dk Raphael Chegeni na Johari wakishindwa kurejea kutokana na kubanwa na majukumu mengine.