Afya: Njia tano za kulinda figo zako

 


Figo zako ni kiungo muhimu sana katika mwili. Hufanya kazi ya kuondoa uchafu katika damu na kutengeneza mkojo.

Pia figo husaidia kudhibiti shinikizo la damu na kudumisha uwiano wa kemikali. Vilevile, hutengeneza seli nyekundu za damu.

Lakini watu wengi hutekeseka kutokana na figo zao kushindwa kufanya kazi na kushambuliwa na magonjwa yasiyokuwa kuambukiza.

Wataalamu wa matibabu wanasema kiwango cha ugonjwa wa figo katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kinatisha. Watu hutumia pesa nyingi kwa ajili ya matibabu na kusafisha figo.

Gharama za matibabu ya figo kwa wastani barani Afrika kwa mtu mmoja ni kati ya dola za kimarekani 13k - 25k.

Wagonjwa wamekuwa wakitegemea usafishwaji angalau mara mbili kwa wiki ili kuishi. Kwa kuondolewa uchafu na maji yaliyozidi katika figo kwani figo haiwezi tena kufanya hivyo. Miongoni mwa wazee na vijana, ugonjwa wa figo umekuwa ukiwamaliza.

Wakati ulimwengu unaadhimisha siku ya figo tarehe 14 Machi, wataalamu wanatufundisha jinsi tunavyoweza kulinda figo zetu.

Njia tano za kulinda figo zako

Dkt. Michael Baah Biney, daktari na mshauri wa masuala ya afya nchini Ghana, anasema kila mtu anapaswa kufanya mambo haya.

Kunywa maji mengi kwa siku

Ukiwa na takriban vikombe 8 vya maji ya kawaida ya kunywa kwa siku, maji yatalinda figo, haswa kwa wagonjwa walio na hatarini kama vile wagonjwa wa kisukari, shinikizo la damu, ugonjwa wa seli mundu.

Punguza pombe na acha sigara

Kupunguza au kuacha kabisa pombe na sigara ni muhimu ili mtu kuziweka figo zake katika afya. Pombe na sigara ni maadui wa figo.

Tumia dawa kwa usahihi

Unapaswa kumuuliza daktari wako kuhusu matumizi ya dawa. Baadhi ya dawa zinaweza kuharibu viungo vyako, hasa figo. Tafuta ushauri wa matibabu na usinunue dawa mtaani.

Fanya vipimo vya tumbo

Kitu kingine ambacho kila mtu anapaswa kufanya, ni vipimo vya tumbo angalau mara moja kila baada ya miaka miwili hadi mitano. Ili kuangalia afya ya figo na viungo vingine.

Fanya mazoezi ya mwili

Tumia dakika 30 au zaidi kwa siku kufanya mazoezi. Husaidia kurekebisha kalori zako na kubaki katika uzito mzuri.

Chanzo: BBC SWAHILI -X


Powered by Blogger.