EWURA YAPONGEZWA KWA KAZI NZURI YA UDHIBITI
Na Penina Malundo, DAR ES SALAAM
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba aipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA ,kwa kazi kubwa inavyofanya ya kudhibiti upatikanaji wa huduma ya Umeme,Gesi Asilia pamoja na Mafuta kwa namna zinavyotolewa kwa ubora.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara''Sabasaba''amesema wizara yake inahakikisha kwamba Mamlaka hiyo inafanya kazi yake kulingana na sheria na sera zilizopo na kuiwezesha EWURA kuweza kutekeleza majukumu yake katika mazingira yanayokubalika ndani ya sekta.
Amesema EWURA inafanya kazi nzuri sana hadi sasa.''Kama mnavyoona huduma zinazodhibitiwa na EWURA zinapatikana na wameweza kudhibiti upatikanaji wa huduma zenyewe ,bei ya huduma inayotolewa na ubora wa huduma hizo,''amesema na kuongeza
''Katika eneo la bei mnafahamu kwamba nchi yetu ni miongoni mwa nchi zenye bei ya chini sana za bei ya umeme hata ukilinganisha na nchi za majirani zetu,Siku za hivi karibuni nyie mashahidi mmeona namna gani ubora wa huduma ya umeme zilivyoimarika sana kule kukatikakatika sana na mgao wa umeme umepungua kwa kiasi kikubwa,''amesema Mhandisi Mramba .
Amesema hii inatokana na wajibu wa EWURA katika kudhibiti kusimamia utoaji wa huduma hizo ambapo hata katika Gesi Asilia mamlaka hiyo imesaidia katika kufatilia na kutoa leseni kwa wale wanojenga vituo vya gesi katika eneo moja (CNG)na vituo vya mafuta lakini anasimamia huduma zinazotolewa na vituo vinakidhi mahitaji ya jamii.
Amewasihi watanzania kufika katika bada lao na kuona huduma wanazotoa ikiwemo huduma ya ushauri na kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuyafanyia kazi.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dk. James Mwainyekule,amesema mwezi uliopita EWURA ilisaini mkataba na Shirika la Umeme nchini Tanesco kupima utendaji kazi na namna ya utekelezaji wa kazi.
" Tunazingati bei katika soko la dunia tukifuatilia na kila mwezi bei zikishuka na kupanda kulingana na soko la dunia linavyoenda,kama majukumu yetu yanavyotutaka kuhakikisha tunadhibiti na kusimamia ubora wa bidhaa ya Umeme na gesi asilia.
Amesema hadi sasa magari takribani 5,000 yanatumia gesi ,hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza dola kutumika katika kiagiza mafuta nje, kwa sababu gesi hii ya mafuta inatoka nchini.