FCC YATOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU BIDHAA BANDIA

 


Na Mwandishi wetu,Mwangwinews

TUME ya Ushindani nchini (FCC) imeendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi  kuhusu bidhaa bandia  na kuhakikisha  mwananchi yeyote haumizwi na bidhaa zisizo na ubora.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao lililopo katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere,Mkurugenzi Mtendaji wa FCC, William Erio amesema FFCC itahakikisha inaendelea kusimamia  sheria ya ushindani nchini inayodhibiti bidhaa hizo.

Erio amesema majukumu yao ni pamoja na kutoa elimu kwa watu kutokufanya Biashara Bandia na kuharibu ushindani wa biashara, "Sisi FCC tutaendelea kuchukua hatua kwa yeyoye atakayebainika kufanya hivyo,"amesema Erio.



Pamoja na hayo amewataka wafanyabiashara na wawekezaji kabla ya kufanya biashara nchini watembelee FCC kwa lengo la kupata elimu .

"Na sisi tunatumia maonesho haya pamoja na kueleza kazi kwa Umma,tunatumia maonesho haya pia kunawashauri kutofanya Biashara Bandia pamoja kutoweka bei kubwa itakayomuumiza mlaji,"

"Tunawakaribisha kwenye Banda hili, tutatoa elimu kipindi chote cha maonesho, hivyo niwakaribishe Wafanyabiashara na wananchi Kwa ujumla waweze kutembelea banda letu," amesema Erio.

Hata hivyo, amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu sahihi kwa uwekezaji kutokana na sera nzuri ikiwemo kuwepo kwa Mamlaka inayodhibiti bidhaa bandia.


Powered by Blogger.