JINSI YA KUCHAJI SIMU WAKATI HAKUNA UMEME

 


Wakati wa majanga kama vile dhoruba, mafuriko na matetemeko ya ardhi, matatizo mengi hutokea kutokana na kukatika kwa umeme.

Katika hali kama hiyo, ikiwa simu haina chaji, ni kama kukata uhusiano na ulimwengu.

Hata tunapokwenda maeneo ya mbali ya milimani, ambako umeme haupatikani, mara nyingi tunakabiliwa na tatizo la kukosa kuchaji simu zetu.

Lakini hata kama huna kifaa cha kuhifadhia chaji (power bank), unaweza kuchaji simu yako ya mkononi kwa urahisi katika hali ya dharura kama hiyo.

Nini kinahitajika?

Mambo machache yanahitajika ili kuchaji simu ya mkononi wakati hakuna umeme:

Waya wa kuchaji simu (USB) na soketi ya gari ya kuchaji

Kebo inayotumika kuchaji simu

Betri ya volteji 9

Kalamu au ufunguo.

Tunachopaswa kufanya ni kupeleka umeme kutoka kwenye betri hadi kwenye simu ya mkononi.

Umeme hutumwa kutoka katika betri hadi kwenye kwa kutumia kiunganishi cha umeme. Hapa ufunguo ndio utakuwa kiunganishi chetu.

Molekyuli za umeme zilizochajiwa hutumwa kutoka kwenye betri hadi kwa simu ya rununu kupitia kifaa kinachowezesha umeme kupitia kati yake.

Hapa klipu ya chuma hutumika kama kifaa hicho kinachowezesha umeme kupitia katikati yake.


Angalau nishati ya kutosha inapatikana ili kupiga simu za dharura na kutuma ujumbe.

Hata hivyo, tujifunze kufanya hivyo katika hatua tatu.

1: Fungua klipu ya chuma na uifunge kwenye nguzo moja ya betri

Betri zina nguzo mbili. Moja ina ishara + (chanya) na nyingine ina ishara – (hasi).

Nguzo hizi mbili zinapounganishwa na waya, elektroni husafiri kutoka katika nguzo hasi hadi kwenye nguzo chanya haraka iwezekanavyo.

Tunatumia kifaa cha chuma ili kuzalisha nguvu hizi za umeme.

Chuma husaidia kupitisha umeme, hatua inayosaidia elektroni kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Vilevile tunafungua klipu ya chuma na kuifunga karibu na nguzo hasi ya betri.

Kama inavyoonyeshwa kwenye picha hii, klipu ya chuma ina upande mmoja unaofunguka kuelekea juu na vilevile kuna upande mwingine unaofunguka kwa nje.

2: Weka adapta ya gari kwenye nguzo chanya ya betri

Baadaye, weka adapta ya gari kwenye nguzo hasi ya betri.



Sasa iko tayari kutoa nguve ya umeme.

3: Gusisha klipu ya betri katika sehemu ya chuma iliyo upande mmoja wa adapta

Kilichosalia ni vyuma hivi viwili kukutana.

Unapogusisha klipu ya chuma - na sehemu ya chuma kwenye adapta matokeo yake ni kwamba,

umeme husafiri kutoka upande mmoja hadi mwengine na hivyo basi unazalishwa

Hatimaye.. simu ya mkononi inapaswa kuchomekwa kwenye soketi ya USB.

Hii inapaswa kuchomekwa sawia na jinsi inavyochomekwa katika kompyuta .

Betri zote zina elektroliti na kemikali nyingine. Zinapogusana husababisha elektroni kusafiri kutoka upande moja hadi mwingine hatua inayosababisha kuzaliwa kwa umeme.

Bila elektroni hizi hatuwezi kuhifadhi nishati katika vifaa vidogo.

Vifaa hivi kama vile betri hutupatia umeme wakati wa hali ya dharura.


Hii ni njia mojawapo ya kuchaji simu yako ya mkononi kwa kutumia vitu vya nyumbani wakati umeme umepotea.

Ukitazama mtandao utapata mawazo mengi kama haya.

Lakini sio yote yanayofanya kazi kwa kufuata kanuni hizi.

Chanzo: BBC SWAHILI-X


Powered by Blogger.