KAIRUKI AITAKA TAWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU KATIKA UTENDAJI KAZI
MOROGORO: Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) wmetakiwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo katika kuongeza tija na kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka hiyo.
Rai hiyo imetolewa leo Julai 8,2024 na Waziri wa Maliasili na Utali, Mhe. @AngellahKairuki (Mb.) katika kikao chake a Menejimenti ya TAWA kilichofanyika Ofisi za Makao Makuu ya TAWA Mkoani Morogoro.
Waziri Kairuki ametumia fursa hiyo kutoa onyo kwa Askari Uhifadhi wanaofanya vitendo visivyofaa katika maeneo yao ya kazi na kuelekeza wafuatiliwe na kuchukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.
“Tujitahidi kudhibiti vitendo visivyofaa kwenye maeneo yetu, pasiwe na uvamizi wa aina yoyote,” amesisitiza Waziri Kairuki.
Aidha, Waziri Kairuki ameonya tabia ya watumishi wanaochelewesha huduma kwa wadau.
“Kila mmoj4a akajichunguze wapi ameshiriki katika kuchelewesha utoaji huduma na kutofuata taratibu hasa katika utoaji wa vibali na nambari za malipo," ameongeza.
Kuhusu minada ya vitalu vya windaji, Mhe. Kairuki amewataka kufanya minada hiyo kwa wakati kwa kufuata kalenda na pia kujifunza kutokana na matokeo ya minada iliyopita kama kulikuwa na changamoto waangalie namna ya kuzitatua, nini cha kuboresha na hadhi za vitalu wanavyovinadi ili kuongeza mapato ya Serikali.
Katika hatua nyingine, Mhe.
Kairuki ameitaka TAWA kuwa na mango mkakati wa kuongeza makusanyo kwa kunadi maeneo yao ya uwekezaji kwenye maonesho wanayoshiriki huku Wizara ikiendelea na mchakato wa kurekebisha kanuni mbalimbali na masuala ya tozo.
Pia Waziri Kairuki ameitaka menejimenti ya TAWA kuwa na utaratibu wa kujengea uwezo watumishi ili waweze kutimiza wajibu ipasavyo katika kumarisha ulinzi ,doria na kupambana na ujangili katika maeneo ya hifadhi.
📸: W/Maliasili na Utalii