LIPIENI GHARAMA ZA KUPIMA ARDHI MPEWE HATIMILIKI- KAMISHNA

 


Na  Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM

KAMISHNA wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, Shukrani Kando ametoa wito kwa wananchi  kulipia gharama za upimaji ardhi ili waweze kupimiwa Viwanja vyao na kupewa Hatimiliki.

Wito huo jana  katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) " Sabasaba" amesema ni muhimu kupata hatimiliki kwaajili ya ulinzi wa ardhi zao kwa kuhakikisja wanapima ardhi.

Amesema kwa sasa   migogoro imekuwa  mingi hivyo mtu  asipokuwa na ulinzi wa kisheria kwenye ardhi yako anaweza akajikuta ameipoteza ardhi yake.

Amesema wamekuwa wakishauri mara kwa mara kwa wananchi kufata taratibu za upimaji wa ardhi ili kupata Hatimiliki itakayowatambulisha  wao ni wamiliki halali wa maeneo yao.

"Tumekuwa tunawashauri wananchi ambao wanamiliki Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na sehemu yoyote ile nchini wajitahidi sana kulipia gharama za upimaji kupitia makampuni ya urasimishaji au taasisi binafsi au ofisi za wakurugenzi, ili wapimiwe ardhi zao na baada ya hapo wapewe hatimiliki zao,"amesema.

Aidha ametoa ushauri kwa wanaouziana ardhi kuhakikisha fedha za malipo zinawekwa katika akaunti ili kuepuka utapeli.

"Haiwezekani kuuza ardhi ya Sh. milioni 200 kwa milioni 50, lazima ujiulize ni kwanini auze kwa bei hiyo? usinunue ardhi kwa kuwa inauzwa kwa bei ya chini unatakiwa kujiridhisha kwanza na fedha zote ambazo unanunua ardhi zipitie kwenye akaunti ya wauzaji,"amesema 

 


Amesema miongoni mwa mikoa inayoongoza mauzo mengi wananchi wanapeana fedha mkononi ni pamoja na mkoa wa Pwani ambapo hali inayopelekea wananchi kutapeliwa kwa kiasi kikubwa.

"Unapouza kiwanja na kupewa hela mkononi  inakuwa ngumu kuthibitisha kwa sababu watu wengi wanakimbia na muda mwingine wanawageuka kwamba haukunipa fedha,hivyo ni muhimu fedha hizo kuingia benkiili kuwepo kwa ushahidi " amesema

Powered by Blogger.