"MAHINDI YANUNULIWE SH.700 KILO MOJA" - DKT. SAMIA AAGIZA

 


Na Mwandishi Wetu

RUKWA: Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Kilimo iliyo chini ya Waziri Hussein Bashe, kuanzia kesho Julai 18 inunue mahindi ya wakulima kwa bei ya shilingi 700 kwa kilo moja badala ya 600  iliyokuwepo kabla ya tamko hilo.

“Nimekuja Rukwa, bado malalamiko ya bei ya mahindi ni mengi. Nilikua nanong’ona  na Waziri wa Kilimo, nikamuuliza kama tunaweza kwenda na bei ya 700, akaniambia Mama ngoja nikapige mahesabu" amesema Dkt.Samia na kuongeza;

"Lakini pamoja na kupiga mahesabu, nakuagiza Waziri, nendeni na bei ya sh.700, na huo ndio usikivu wa Serikali

Kuanzia kesho NFRA(Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula) wakifungua kesho ni 700, yale mengine Waziri utajua tofauti unaitoa wapi.” 

Agizo hilo na mengine ameyatoa leo mkoani Rukwa anakoendelea na ziara ya kikazi ya kuwatembelea wananchi na kuzindua miradi ya maendeleo.



Powered by Blogger.