POLISI 4 WAFUKUZWA KAZI
DODOMA; Jeshi la Polisi Tanzania limewafukuza kazi askari wake wanne wa kitengo cha usalama barabarani kwa sababu iliyoelezwa kuwa ni vitendo vya ukiukaji wa miongozo na taratibu za kazi.
Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa Jeshi hilo DCP David Misime inaeleza, askari hao walikutwa na hatia baada ya kuchezea mfumo wa kamera za Jeshi za kuangalia mwendokasi(speed radar) , kwa kufuta kumbukumbu za madereva waliokuwa wanaendesha magari kwa mwendo kasi.
Tukio hilo lilifanyika Wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro Mei 30,2024
Aidha, taarifa hiyo ambayo haikutaja majina ya askari hao, imeeleza, kabla ya kufutwa kazi, walishtakiwa kijeshi na kukutwa na hatia