VETA YAENDELEA KUWEKEZA UJENZI WA VYUO VYAKE NCHINI

 



Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM 

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),  imesema Serikali inaendelea kuwekeza ujenzi wa vyuo vya VETA kuanzia Wilaya hadi Mikoa ikiwa na lengo ya kutoacha nyuma watu wote kwenye kupata mafunzo ya ujuzi.

Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore amesema wao wanataka vijana wote nchini wapate ujuzi ambao unakwenda kuwa fursa kwao katika kuendesha maisha yao.

Amesema kupitia maonesho haya  kuna Ubunifu wa Teknolojia mbalimbali ambazo zinakwenda kutatua changamoto katika sekta zote za kiuchumi.


Amesema wanakwenda na Sera ya Serikali ya kuwa wanafunzi wote wanafika kidato cha nne ambapo watapata kusoma  mafunzo ya ujuzi hapo ndipo VETA kuwa na kutengeneza Walimu watakwenda kuwafundisha ujuzi.

CPA Kasore amesema kuwa vijana wa Tanzania katika maeneo yote vyuo vya VETA vimejengwa waende kupata mafunzo ya ujuzi ambapo watakuwa wameondokana na tatizo la ajira kutokana na fursa zilizopo katika maeneo yao.

Amesema katika kuwa Kilimo ni Uti wa mgongo ambapo wanaotaka kufanya Kilimo watapata mafunzo na ujuzi na Kilimo cha uhakika na sio Kilimo cha kubahatishaa hali kadhalika kwa Sekta mifugo na Uvuvi wafanya hivyo hivyo.

Aidha amesema katika kuwa VETA katika kutambua changamoto ya makundi Maalum VETA inachukua na kupata mafunzo ambapo matokeo yake hadi sasa yamekuwa chanya na kutoa wito wa jamii kuacha kuwafungia ndani kwani kufanya hivyo ni kuwakosesha fursa za msingi kwa kundi hilo.

CPA Kasore amesema sio vijana pekee wanaweza kupata mafunzo hayo hadi wastaafu wanaweza kupata mafunzo hayo ya ujuzi na kuweza kuendelea kuzalisha bila kutegemea mafao ya ustaafu.

Powered by Blogger.