MADAKTARI WA RAIS SAMIA WALIVYO IBUA MAKUBWA KWENYE HALMASHAURI 184

 


Na WAF - Dar es Salaam 

Zoezi la utoaji wa huduma za kibingwa kwenye Hospitali 184 ngazi ya Halmashauri kupitia mpango kabambe wa "Madaktari bingwa wa Dkt. Samia limepunguza mateso na kukomboa wagonjwa wengi, hasa wale walioteseka kwa ugonjwa wa uvimbe wa muda mrefu. 

Waziri wa Afya ,Ummy Mwalimu amesema hayo leo Agosti 7, 2024 wakati akitoa taarifa juu ya madaktari bingwa wa Rais Samia kwa waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam. 

"Tumeshuhudia mawe yakiondolewa kwenye vibofu vya mikojo ikiwemo jiwe la ukubwa wa kilo 1 na gram 200, upasuaji wa Goita, watoto 20 wamefanyia upasuaji wa kurekebisha maumbile ya uume (hypospodiasis repair) ambayo yangeweza kusababisha ulemavu wa kukudumu.amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amesema katika zoezi hilo takribani wagonjwa elfu 70 wamefikiwa ambapo kati yao, madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani waliona wagonjwa 22,057 sawa na aslimia 32, magonjwa ya wanawake na uzazi 18,044  sawa na asilimia 26 watoto 14,466 sawa na asilimia 21 na madaktari bingwa wa upasuaji waliona wagonjwa 10,578 (15%), Kwa ujumla wateja 4,652 sawa na asilimia 7 walipata huduma za upasuaji.


Amesema, Mikoa 10 iliyoongoza kwa wagonjwa wengi waliojitokeza kuonwa na madaktari bingwa wa Rais Samia ni mkoa wa Tanga wateja elfu 4,410, Mara wagonjwa 3,671, Tabora 3,652, Mtwara 3,540, Mwanza 3,256, Ruvuma 3,253, Mbeya 3,126, Kagera 3,122, Pwani 2,966 pamoja na Manyara wagonjwa 2,964.

"Zaidi ya hayo tumebaini, kati ya watoto 14,466 walioonwa, matatizo ya mfumo wa hewa na moyo yaliongoza kwa kuwa na wagonjwa 2,352 sawa na asilimia  16, uambukizo wagonjwa sawa  2,091 sawa na asilimia 15, upungufu wa damu au Sickle Cell wagonjwa 1,287 sawa ha asilimia 9 na Nimonia wagonjwa 1,030 sawa na asilimia 7 ." Amesema Waziri Ummy.


Powered by Blogger.