TAARIFA MBILI KUTOKA NCHI MBILI KUHUSU BANGI
TAARIFA KUTOKA RWANDA
Ujenzi wa kiwanda cha kusindika bangi katika Wilaya ya Musanze, nchini Rwanda umefikia asilimia 70% hadi sasa huku mradi huo ukitarajiwa kukamilika mwezi septemba mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa KKOG Rwanda, Rene Joseph ameliambia gazeti la New Times la Rwanda na kuongeza kuwa ujenzi huo umechelewa kutokana na changamoto ya miundombinu ya barabara.
Machi 2024, Serikali ya Rwanda ilitoa leseni ya miaka 5 ya kulima bangi kwa madhumuni ya dawa, uchimbaji na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali za dawa kwa kampuni ya King Kong Organics (KKOG-Rwanda) inayoshirikiana na Shirika la Marekani la KKOG GLOBAL ambalo dhamira yake ni kuwa kinara wa soko katika kilimo cha bangi ya matibabu katika Bara la Afrika.
Bodi ya maendeleo nchini humo (RDB) imetenga eneo la hekta 35 katika Wilaya ya Musanze kwa Wawekezaji watano ambao wameonesha nia ya kuzalisha bangi ambapo pia Serikali ya Nchi hiyo pia imejitolea kutoa miundombinu kama vile barabara, umeme, uzio wa maeneo ya kilimo, kamera za uchunguzi ili kuzuia bangi kuingia mtaani kwa Wananchi.
Katika mwaka wa fedha wa 2023/2024, Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB) ilitenga fransi za Rwanda (Rwf) milioni 700 (Tsh. bilioni 1,428,000,000) kwa mradi wa kilimo cha bangi ambapo kwa mwaka 2024/2025, bajeti iliongezwa hadi kufikia fransi za Rwanda (Rwf) bilioni 2 (Tsh. bilioni 4,080,000,000) ambapo hekta 1 ya bangi inatarajiwa kuzalisha hadi dola milioni 10.

TAARIFA KUTOKA TANZANIA
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imeteketeza jumla ya ekari 1,165 za mashamba ya bangi na kukamata kilogramu 102 za mbegu za bangi ikiwa ni matokeo ya oparesheni maalum Mkoani Morogoro iliyofanyika kwa siku tisa
katika vijiji vya Nyarutanga, Lujenge na Mafumbo vilivyopo Wilaya za Morogoro vijijini na Kilosa ambapo katika vijiji vya Mafumbo na Lujenge
Katika oparesheni iliyofanyika kijiji cha Nyarutanga Watu 6 wakiwa na kilogramu 342 za bangi wamekamatwa na watafikishwa Mahakamani taratibu za kisheria zitakapokamilika.
Akiongea baada ya uteketezaji wa mashamba hayo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, mashamba ya bangi yaliyoteketezwa yamelimwa pembezoni mwa Mto Mbakana, Misigiri na Mgeta kwenye eneo la akiba la Hifadhi ya Taifa Mikumi.
Lyimo amewashukuru sana Wananchi hususan Vijana waliojitolea kushiriki katika zoezi zima la uteketezaji wa mashamba ya bangi.
Picha kwa hisani ya HayoTv