BOBI WINE APIGWA RISASI
KAMPALA: Mwanasiasa na kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uganda cha NUP Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine anadaiwa kupigwa risasi ya mguu na vikosi vya usalama vya nchini humo.
Taarifa ilitolewa hivi punde katika mtandao wake wa X(twitter) inasema;
"Jioni hii wakati Rais wetu akirejea kutoka Bulindo katika Manispaa ya Kira alikokuwa amekwenda kuonana na mmoja wa wanasheria wetu, Musisi George, polisi na wanajeshi chini ya uongozi wa Twesigye walizingira magari yetu na kuanza kufyatua risasi za moto, vitoa machozi na virungu.
"Katika harakati hizo, Rais wetu Bobi Wine ambaye ni dhahiri alilengwa alipigwa risasi ya mguu. Kwa sasa anahudumiwa na timu ya madaktari"