BREAKING: 'MEYA' AFIKISHWA KORTINI
-Akosa dhamana, arejeshwa mahabusu hadi Jumatatu Septemba 23
DAR ES SALAAM: Aliyekuwa meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob tayari amepandishwa kizimbani leo Alhamisi Septemba 19, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaama alikosomewa mashtaka mawili yanayomkabili ya kuchapisja taarifa za uongo kinyume na sheria ya makosa ya mtandao.
Kosa la kwanza linalomkabili Boniface Jacob linahusu kuchapisha taarifa za uongo mnamo tarehe 12 Septemba 2024, ambapo alidai kuwa Mafwele anatuhumiwa na familia nyingi kwa kupotea kwa wanafamilia wa hizo familia.
Kosa la pili, ambalo lilitokea tarehe 14 Septemba 2024, linahusiana na kuchapisha taarifa nyingine za uongo zinazosomeka ‘Polisi wanatesa watu na kuua ndio kazi wanaweza’. Boniface amekana mashtaka yote hayo.
Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Nasoro Katuga, pamoja na wenzake watano, umeiomba Mahakama ya Kisutu kumtaka mtuhumiwa Boniface Jacob kuruhusu wapelelezi kuingia kwenye simu zake za mkononi na akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) ili kukamilisha upelelezi unaohusiana na makosa hayo ya kimtandao.
Aidha, Wakili wa Serikali aliiomba Mahakama izuie dhamana ya mtuhumiwa kwa ajili ya usalama wake. Ombi hili lilitolewa na mwendesha mashtaka kwa hoja kuwa kuna hatari za kiusalama endapo mtuhumiwa ataachiliwa kwa dhamana.
Jopo la mawakili wa utetezi linalowakilisha maslahi ya Boniface Jacob linaoongozwa na Wakili Peter Kibatala, pamoja na Wakili Hekima Mwasipu
Boni Yai alikamatwa jana Jumatano, maeneo ya Sinza na Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kumpeleka Kituo cha Polisi cha Osterbay. Kisha usiku wa jana alipelekwa nyumbani kwake Mbezi Msakuzi kwa upekuzi.
Jopo la mawakili sita (waliofika muda huu) likiongozwa na Mhe Peter Kibatala, tayari lipo hapa katika Mahaka ya Mkazi Kisutu kwa ajili ya kumtetea Mhe Boniface.Saa 12:04 jioni