KIKOSI CHA YANGA KILICHOELEKEA ETHIOPIA

 


Hiki ni kikosi cha wachezaji wa  klabu ya Young African SC kilichoondoka alfajiri ya leo kuelekea Ethiopia kucheza mchezo wa Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya CBE SA

Kikosi hicho hakikuwajumuisha beki Nickson Kibabage na kiungo Farid Mussa.

Kibabage hakujumuishwa kutokana na kufiwa na baba yake mzazi 


Naye Farid hatakuwemo kwenye skwadi kufuatia majeraha yaliyosababisha afanyiwe upasuaji wa misuli iliyochanika nyuma ya goti na madaktari wanasema atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili hadi mitatu. 

Pichani: Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Said akimjulia hali mchezaji Farid Mussa Malik Haspitalini anakoendelea na matibabu. 




Powered by Blogger.