WAHOLANZI WAWANOA MAKOCHA WA TIMU ZA MAJESHI

 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi (CDF),Jenerali John  Mkunda kupitia Uratibu wa Baraza la Michezo la Majeshi ya Ulinzi Dunia(CSIM),imewaleta Wakufunzi na Wataalum wa masuala ya Ukocha wa mpira wa miguu kutoka nchini Uholanzi kwa lengo la kutoa mafunzo kwa Makocha Wanajeshi na Askari wa nchini Tanzania.

Mafunzo hayo yatatolewa ndani ya wiki mbili kwa lengo la kuwafua makocha hao na kuwa walimu wazuri watakaosaidia timu zao za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zinazoshiriki ligi mbalimbali nchini na za Taifa.

Dhamira ya CDF ni kuhakikisha kunakuwepo na  walimu wazuri watakao saidia timu zao ndani ya Jeshi pamoja na kuongeza mahusiano mazuri kati ya Tanzania na nchi ya Uholanzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti makocha ambao ni Maafisa wa JWTZ na Askari wamemshukuru CDF kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo kwa makocha na kwamba  wakufunzi wa TFF wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali kwao lakini walimu hao wakigeni wana ujuzi zaidi ambao wataweza kuuongezea.


Wamesema watahakikisha ndani ya kipindi cha mafunzo haya watafanya vizuri  katika kuhakikisha timu za majeshi na Taifa zinafanya vizuri.

Mafunzo  haya ni ya wiki mbili ambapo Septemba 13 mwaka huu yanatarajiwa  kufungwa  rasmi,mafunzo haya yanatokana na mahusiano mazuri ya Chama Cha Mpira wa miguu Cha majeshi .

Powered by Blogger.