JAFO AMEITAKA BODI MPYA YA WAKURUGENZI FCC KUFANYIA KAZI CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI NCHINI


Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM 

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Suleiman Jafo ameitaka Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Tume ya Ushindani( FCC) kufanya vikao vya haraka ili kupitia mambo yote yanayotakiwa kupatiwa ufumbuzi katika masuala ya uwekezaji Nchini.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo leo Oktoba 4,2024 Jijini Dar es salaam wakati akizindua bodi hiyo,kwani bodi hiyo inajukumu kubwa la kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika maono yakuvutia wawekezaji na kukuza Uchumi wa Taifa Nchini.

" FCC ni injini ya uwekezaji Nchini,hivyo bodi hiyo mpya itasaidia Wizara ya Viwanda na Biashara katika kuhakikisha sekta Binafsi inakua kwa kasi nakuleta mchango wa Maendeleo pamoja na kuondoa changamoto ya ajira kwa Vijana"amesema Waziri Jafo



Amesema kwamba wakati mwingine makampuni yanahitaji kuungana ,lazima upembuzi wa haraka uwepo ili kuona je Muungano huo una tija kwa Taifa na kama una tija basi mfanye mchakato ufanyike kwa haraka.

Aidha ameongeza kuwa sekta binafsi ndio suluhisho la kujibu mahitaji ya ajira kwa Vijana wanaohitimu kila Mwaka ,na jukumu hili tumepewa sisi Wizara ya Viwanda na Biashara, hivyo naomba FCC mfanye kazi yenu kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.

Hata hivyo Waziri Jafo amewashauri watendaji wa FCC kufanya kazi kwa kuzingatia mabadiliko ya sheria katika kufanya tathmini ya namna makampuni yanavyoweza kuungana ili kuleta tija katika ushindani kibiashara.

 Waziri huyo wa Viwanda na Biashara amewataka watendaji wa Tume ya Ushindani kutoa ushirikiano wa dhati kwa Bodi ya Wakurugenzi ili iweze kufanya kazi nakufikia malengo waliyojiwekea na kwamba bodi hiyo isipofanya kazi zake vizuri inaweza kuiyumbisha Serikali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa maono ya kuweka mazingira rafiki na tulivu ya ufanyaji Biashara Nchini.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya FCC Dkt.Aggrey Mlimuka amemhakikishia Waziri Jafo kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa Bodi hiyo.

"Mheshimiwa Waziri nikuhakikishie kwamba tutafanya kazi hii kwa weledi na kutekeleza yale yote ulioagiza na Bodi hii itajitahidi kumsaidia Rais wetu ili kuvutia wawekezaji wengi katika kuleta ushindani kwa Taifa letu",amesema.

Powered by Blogger.