NDEGE YA KWANZA KUUNDWA TANZANIA YAPAA KWA MARA YA KWANZA

 Ndege ya kwanza kati ya tatu zilizotengenezwa  Morogoro,nchini Tanzania, imekamilisha safari yake ya kwanza kwa mafanikio, na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 Ndege hiyo aina ya Skyleader 600, imepata idhini kutoka kwa mamlaka zinazohitajika baada ya kukaguliwa kwa ubora na sasa iko tayari kufanya kazi katika njia za ndani na nje ya nchi.

Kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL), iliyoendesha mradi huo, ilianzisha kiwanda hicho nchini Tanzania kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji nchini. Ndege za Skyleader 600 zimeundwa kwa matumizi ya kibinafsi na ya kibiashara, na kutoa suluhisho jipya la usafirishaji kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.


Hii ni hatua kubwa na muhimu kwa Tanzania inapoingia katika sekta ya utengenezaji wa ndege



Powered by Blogger.