POLISI WAKABIDHIWA MAGARI 77
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelikabidhi Jeshi la Polisi magari 77 kwa ajili kurahisha utekelezaji wa majukumu yake ya kusimamia usalama wa raia na mali zao ikiwa ni mwendelezo jitihada za Serikali kulifanya Jeshi hilo kuwa la kisasa lenye vifaa, na weledi wa kuzuia uhalifu.
Akikabidhi magari hayo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Waziri Masauni amelitaka Jeshi hilo kuhakikisha kuwa linayatumia vyema magari hayo kwa kupunguza malalamiko ya wananchi dhidi ya Jeshi la Polisi