TEA YAZINDULIWA RASMI

 


Na Mwandishi wetu,DAR ES SALAAM 

SERIKALI imeipongeza Chama cha Wataalamu na Wadau wa Nishati nchini (TEA) kwa uanzilishwi wake huku ikiwasisitiza kufanya kazi kwa miongozo,sera na taratibu ambazo serikali inaziandaa katika upande wa Nishati.

Pia kimewapongeza kwa jitihada zao mchango mkubwa wa kuwaunganisha wadau mbalimbali wa nishati nchini katika kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili za masuala ya nishati.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwaniaba ya Waziri wa Nishati,Deogratius Ndejembi,Mwakilishi wa Wizara hiyo Emilian Nyanda alisema TEA inaendeleza jitihada ya Sekta ya Nishati katika kufanya kazi yake.

Amesema kama wizara inahitaji wadau ambao watashirikiana nao katika kusukuma gurudumu la nishati kutokana na sekta hiyo kuwa muhimu katika nchi."Kwani sote tunajua umuhimu wa sekta ya nishati,sasa unapokuta mdau kama Chama hiki cha nishati nchini ni muhimu sana katika kushirikiana na serikali katika kuendeleza ajenda za upatikanaji wa nishati.

"Nishati inayozungumziwa sio umeme pekee bali nishati zinazozungumziwa ni pamoja na nishati safi ya kupikia ,matumizi bora ya nishati na sekta ya usafiri'"amesema Nyanda

Amesema wanamuangalia TEA kama mdau muhimu katika kusaidiana kutekeleza ajenda zao za nishati hivyo wameongeza wigo wa wadau katika kujega uwelewa juu ya msuala ya nishati. "Tunatarajia TEA itusaidie katika kuwafikia wadau wengi zaidi na kushughulika na masuala ya utafiti,uvumbuzi itakuwa jukwaa la kubadilishana mawazo na serikali.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama hicho cha TEA, George Michael,amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa chama hicho ni kuwaunganisha wadau wa nishati na kuwafanya kuwa sauti moja itakayowezesha kuwasilisha hoja, changamoto na mapendekezo yao kwa ufanisi, kabla ya kuwasilishwa kwenye wizara husika kwa ajili ya utekelezaji wa sera na sheria.

“Tunawakaribisha wadau wote na vyama mbalimbali vya nishati kuungana nasi, kushirikiana kwa karibu na kuangalia namna bora ya kusukuma gurudumu la maendeleo ili kufikia matumizi makubwa na bora ya nishati, hususan nishati safi inayohitajika sana katika jamii kwa sasa,”amesema George Michael.

Amesema TEA pia itawaunganisha wanachama wake na fursa za kimataifa kupitia ushirikiano na nchi na taasisi mbalimbali duniani, jambo litakalowezesha kubadilishana uzoefu na teknolojia. Kupitia chama hicho, wadau wanaojihusisha na uzalishaji na matumizi ya nishati kama gesi ya magari, petroli, oksijeni, biogesi, umeme wa maji (hydro) pamoja na taasisi kama Tanzania Atomic Energy Commission, watanufaika na mtandao mpana wa ushirikiano na maendeleo.






Powered by Blogger.