MOALIN AREJESHWA YANGA




Uongozi wa Yanga SC umemrejesha kundini Kocha Abdihamid Moalin “kama kocha msaidizi wa Pedro Goncalves”.


Uamuzi huo umefanywa leo katika kikao kilichofanyika makao makuu ya klabu hiyo, Jangwani Dar es Salaam, baada ya kupokea ripoti kutoka benchi la ufundi la timu hiyo. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mara baada ya kikao hicho, uongozi wa Yanga umebaini kuwepo kwa changamoto kubwa mbili ambazo ni kucheza mechi nyingi ndani ya kipindi kifupi (mechi saba ndani ya siku 21), na uwepo wa wachezaji wanane (8) ambao ni majeruhi. 

Kikao hicho pia kimefanya tathmini ya mwenendo wa timu kwenye mashindano mbalimbali msimu huu na kubaini “uwepo wa changamoto ya kiufundi inayoifanya timu icheze aina tofauti ya uchezaji (style of play) na ile iliyozoeleka” 

Mwisho, uongozi wa klabu hiyo umewaahidi wanachama na mashabiki wake kuwa itarejea mzunguko wa pili ikiwa imara na nguvu kubwa kuelekea kutimiza malengo yake ya msimu wa 2025/26 ambayo ni pamoja na kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC pamoja na Kombe la Shirikisho la CRDB Bank

Powered by Blogger.