RC CHALAMILA WAPORAJI ARDHI NA UTAPELI WA AINA YOYOTE DAR KIKAANGONI


-Akemea wimbi la utapeli katika Mkoa huo, aitaka Jamii kutokuwa sehemu ya migogoro.

Na Mwandishi wetu,DAR ES SALAAM 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa muda wa wiki moja kuanzia machi 2,2026 kwa makundi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya utapeli na unyang'anyi wa mali ikiwemo ardhi kujisalimisha kwa kurudisha mali walizozichukua kwa wamiliki halali kwani Serikali mkoani humo imekusidia kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote watakaokiuka agizo hilo

Kauli hii imekuja kufuatia ziara ya mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es salaam wilaya ya Kinondoni kubaini kukithiri kwa vitendo hivyo ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakitumia njia ya kukodisha maeneo na baadae kufanya utapeli

Akizungumza Jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa huo Mhe Albert Chalamila amesema Serikali Mkoani humo imebaini uwepo wa kiwango kikibwa cha utapeli na unyang'anyi wa ardhi na kusababisha vilio na machozi kwa baadhi ya makundi ya watu ikiwemo wajane na warithi.

RC Chalamila ameongeza kuwa Serikali Mkoani humo pia imebaini uwepo wa utapeli kwenye show room za kuuzia magari ambapo watu wamekuwa wakilipia magari na kudhulumiwa kwa kisingizio kuwa magari yao bado yapo bandarini lakini pia Serikali  imebaini uwepo wa mikopo isiyokuwa na tija inayowaumiza wananchi kupitia masharti magumu hivyo anakwenda kuchukua hatua

Aidha RC Chalamila pia ametoa muda wa wiki moja kuanzia machi 2,2026 akiwataka wananchi wote ambao wanamadai ya kutapeliwa ama kudhulimiwa mali zao ikiwemo ardhi kuwasilisha malalamiko yao kwenye ofisi yake kwani amekusudia kufanya ziara maalumu ya kufuatilia na kutatua migogoro hiyo kuanzia machi 9 mwaka huu

Sanjari na hayo RC Chalamila ameipongeza Mahakama na TAKUKURU kwa namna wanavyoshugulikia kesi hizo huku akitoa tahadhari kwa baadhi ya wasimamizi wa mirathi wanaouza mali za warithi halali kwa kisingizio cha kulea ama kisomesha watoto wa marehemu kwani yapo matukio mengi ya warithi kunyimwa haki zao

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila amezungumzia ujio wa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan katika Mkoa huo machi 3, 2026  ambapo anatarajia kuzindua matanki ya kuhifanyia mafuta wilaya ya  kigamboni hivyo amewataka wananchi kukitokeza kwa wingi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.







  

Powered by Blogger.