SENEGAL YAPOKONYWA UBINGWA WA AFCON 2025
Senegal wamevuliwa Ubingwa wa Afrika #AFCON2025 na badala yake CAF imewapa Morocco Ubingwa huo.
Uamuzi huo umetolewa usiku huu kufuatia rufaa ya Morocco waliolalamikia vitendo visivyo vya uana michezo , vilivyofanywa na Senegal katika mchezo wa fainali.
CAF imewapa ushindi Morocco katika rufaa hiyo na 'ushindi wa mezani' wa mabao 3-0, hivyo Senegal kutakiwa kurejesha kombe na medali, ili wakabidhiwe mabingwa wapya, ambao sasa ni Morocco.

