AHMED ALLY AKUTANA NA VIONGOZI WA MATAWI YA ARUSHA KUPANGA MIKAKATI YA HAMASA YA KOMBE LA SHIRIKISHO
Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amekutana na viongozi wa matawi ya Arusha kupanga mikakati ya hamasa kuelekea mchezo wetu wa kombe la CRDB dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa April 12, 2026 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Katika mkutano huo Ahmed amewataka viongozi hao kutoathiriwa na matokeo ya mechi iliyopita baadala yake waongeze nguvu ya kuhamasisha mashabiki katika matawi yao kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili.

