BELARUS YAMWAGA FURSA ZA BIASHARA KWA WATANZANIA KUPITIA TANTRADE*

 






28 Aprili 2026

Dar es Salaam


Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)  imeendelea kuimarisha jitihada za kukuza biashara za kimataifa ambapo imepokea ugeni kutoka Belarus kwa lengo la

kujadili fursa za kukuza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Belarus.


Akizungumza kuhusu fursa zilizopo nchini Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Dkt. Latifa M. Khamis, alieleza kuwa Tanzania ina fursa nyingi za biashara katika sekta mbalimbali ikiwemo Madini, Kilimo, Afya, Usafirishaji na Burudani. 


Kwa upande wa Belarus, Mkurugenzi Mkuu wa 'National Export Promotion Centre, Mheshimiwa,Mikalai Barysevich ameeleza kuwa nchi hiyo ina uwekezaji mkubwa wa teknolojia za viwandani, jambo linalotoa fursa kwa Tanzania kunufaika kupitia teknolojia na utaalamu katika sekta hizo. 

Kadhalika, TanTrade ilitumia fursa hiyo kumkaribisha Mhe. Mikalai pamoja na wadau wa Biashara kutoka Belarus kushiriki katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam yatakayofanyika kuanzia Juni 28, 2026 jijini Dar es Salaam, ikiwa ni jukwaa muhimu la kuonesha bidhaa, huduma na teknolojia mbalimbali.

Mazungumzo haya yamefanyika Makao makuu ya TanTrade jijini Dar es Salaam.



Powered by Blogger.