ELIMU BILA ADA (FAHAMU VIPIMO VYA ARDHI KABLA YAKUNUNUA UEPUKE KUIBIWA)
Watu wengi hununua viwanja na kugundua baadaye kuwa wameibiwa ukubwa au wamepunjwa kiwanja si kwa sababu muuzaji ni mwizi, bali kwa sababu wao hawakuelewa vipimo.
Makosa makubwa yanayowagharimu wanunuzi wengi wa viwanja ni kutokuwa na uelewa au kutofahamu ukubwa halisi wa kiwanja wanachonunua.
Wengi wamezoea tu kusikia tu maneno kama “kiwanja hiki ni 20 kwa 40” bila kujua maana yake kwa upana.
Makala hii imeandaliwa na gulio la ardhi kukusaidia kuelewa kuhusu vipimo vya viwanja ili uweze kujua ukubwa wa kiwanja chako,
Uepuke kudhulumiwa/kupunjwa
Kufanya maamuzi sahihi ya ujenzi na uwekezaji.
Kwa kawaida, ukubwa wa kiwanja hupimwa kwa mfumo wa Upana na urefu.
Upana (Width)
Urefu (Length)
Vipimo hivi hupimwa kwa mita (meters).
Mfano:
Ukisikia kiwanja kina ukubwa wa 20m × 40m
Maana yake ni hii
Upana = mita 20
Urefu = mita 40
Vilevile kupitia vipimo hivyo kuna namna ya Kukokotoa Ukubwa wa Kiwanja (Area) ili kujua jumla ya mita za kiwanja.
Njia rahisi ya kukokotoa ni kama ifuatavyo.
Ukubwa wa Kiwanja = Upana × Urefu
Mfano:
Kiwanja cha ukubwa wa 20m × 40m = 800 Square Meters (SQM)
Ina maana mita 20 upana unazidisha kwa mita 40 urefu unapata kiwanja cha ukubwa wa mita 800.
Yaani hesabu ni kuwa unachukua mita za upana unazidisha kwa mita za urefu unapata ukubwa wa kiwanja.
Mita 10 upana mara mita 20 urefu = unapata kiwanja cha ukubwa wa mita 200
AU
Mita 20 upana mara mita 20 urefu = unapata kiwanja cha ukubwa wa mita 400
AU
Mita 20 upana mara mita 25 urefu = unapata kiwanja cha ukubwa wa mita 500
Hivyo ndio vipimo sahihi vinavyotumika serikalini katika harakati za kukupatia hati ya kiwanja.
Pia ukisikia neno Square Meter ama kifupi chake kama (SQM) ina maana ni eneo la mraba lenye urefu wa mita 1 na upana wa mita 1.
Kwahiyo ukiambiwa square Meter 1 ni sawa na kuambiwa mita moja mara mita moja.
Neno “Square” maana yake ni mraba.
Mraba ni umbo lenye pande 4 ambapo kila upande una urefu sawa.
Kila kona ni digrii 90
Kwa hiyo square meter ni:
Mraba wenye kila upande ni mita 1.
Neno Meter (mita) ni kipimo cha urefu.
Mita 1 ni sawa na hatua moja kubwa ya mtu mzima (hii ni nadharia).
Vilevile unaweza kuhakikisha usahihi wa ukubwa wa eneo kwa kupima mwenyewe kwa namna ifuatayo.
Tafuta Tape measure (kipimo cha mita) na kamba.
Anza kwa kupima upande wa kwanza (urefu)
Kisha pima upande wa pili (upana)
Hakikisha pembe ni sawa (angle ya digrii 90)
Kisha zidisha vipimo ambapo utachukua kipimo cha urefu × kipimo cha upana.
(Hii ni kwa makadirio tu)
Kwa usahihi zaidi na matumizi ya kisheria lazima:
Upime ardhi kwa mpimaji aliyesajiliwa na wizara.
Vipimo Maarufu vya Viwanja Tanzania ni kama vifuatavyo;
10m × 20m=200 SQM
20m × 20m=400 SQM
20m × 30m=600 SQM
20m × 40m=800 SQM
25m × 40m=1,000 SQM
Faida ya kutambua ukubwa wa eneo kwa usahihi hukusaidia Kuchagua ramani inayotoshea katika eneo lako.
Kujua thamani halisi ya kiwanja chako.
Kuepuka migogoro ya mipaka
Kufanya uwekezaji wenye faida
Yaani kujua vipimo vya ardhi ni muhimu kwa kila Mtanzania anayetaka kumiliki ardhi.
Ardhi ni mali ya kudumu ukifanya kosa dogo leo linaweza kukugharimu maisha yako yote.
BASI KWA UJENZI WA UHAKIKA WASILIANA NA INJINIA LAMECK
+255 756 399 084



