NYOTA YA BONGO MOVIE YAZIMIKA: HASHIM KAMBI AZIKWA KISUTU, WASANII WAMLILIA KWA HUZUNINYOTA YA BONGO MOVIE YAZIMIKA: HASHIM KAMBI AZIKWA KISUTU, WASANII WAMLILIA KWA HUZUNI

 



Na Mwandishi Wetu


Mamia ya watu, wakiwemo wasanii, ndugu na marafiki, walijitokeza kumpumzisha katika nyumba yake ya milele msanii mkongwe wa filamu za Bongo Movie, Hashim Kambi. Msafara wa mazishi ulianzia nyumbani kwake hadi katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam, ambapo alizikwa kwa heshima kubwa.


Wasanii mbalimbali walionyesha masikitiko yao kufuatia kifo chake, wakimtaja kama nguzo muhimu katika tasnia ya filamu nchini. Miongoni mwa waliotoa salamu za rambirambi ni mwigizaji mkongwe Charles Magali, ambaye aliandika kwa huzuni:

"Jana ilikuwa siku mbaya sana. Kambi, siamini kama kweli umetutoka.


 Umeondoka mapema mno," akiambatanisha ujumbe huo na kumbukumbu ya picha yao wakiwa pamoja New York.


Hashim Kambi anakumbukwa kama msanii nguli aliyetoa mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza tasnia ya filamu nchini. Kaburi lake lililopo katika makaburi ya Kisutu, katikati ya Jiji la Dar es Salaam, sasa limebaki kuwa kumbukumbu ya maisha na urithi wake katika sanaa.


Pengo lake litaendelea kuhisiwa na wengi waliomfahamu na kupenda kazi zake.

Powered by Blogger.