SERIKALI YAJIPANGA KUREKEBISHA SHERIA ILI ZIENDE SAMBAMBA NA DIRA 2050*

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera amesema kuwa Serikali iko mbioni kufanya maboresho ya sheria mbalimbali ili ziende sambamba na malengo ya Dira Taifa 2050.

Dkt. Homera ametoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano wa Watumishi wa Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali uliofanyika tarehe 28 Aprili, 2026 Jijini Arusha.

*“Nimpongeze Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameanza vizuri na sasa tunaenda kurekebisha sheria mbalimbali ili ziweze kueandana na malengo ya kufikia  Dira ya 2050”.*

Akizungumza katika Mkutano huo, Waziri wa Katiba na Sheria ameeleza kuwa ni muhimu kwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea kujiendeleza kitaalamu na Kimaarifa ili waweze kuishauri vizuri Serikali na kuinua uchumi wa Taifa.

*“Napenda kutoa rai kwenu mzidi kujiendeleza kitaaluma na kimaarifa ili muweze kulishauri vizuri Taifa letu hasa juu ya Sheria zipi zinapaswa kutungwa na kurekebisha kwa ajili ya kuchochea vizuri ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kweli kwa Wananchi wote.”* Amesema Dkt. Homera

Aidha, Dkt. Homera amempongeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Menejimenti ya Ofisi kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

*“Nimshukuru Mhe. Rais kwa kukuteua tena kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali unaitendea haki nafasi hiyo, pia nikupongeze Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali na timu yako kwa maboresho makubwa uliyoyafanya katika Ofisi hii.”* Amesema Mhe. Dkt. Homera. 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari akizungumza awali kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, amesema kuwa ili kufikia malengo ya Dira 2050 ni muhimu kwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakaongeza kasi katika maboresho ya Sheria mbalimbali.

*“Wakati wenzetu wengine wanakuja, wakute tayari tumezifungamanisha sheria zetu na malengo ya Dira 2050 kwa kuzifanya rafiki na wezeshi.*SERIKALI YAJIPANGA KUREKEBISHA SHERIA ILI ZIENDE SAMBAMBA NA DIRA 2050*

*• “Ili kufikia malengo ya Dira 2050 ni lazima sisi tukiwa washauri wa kisheria tukimbie mbele zaidi”- Mwanasheria Mkuu wa Serikali*

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera amesema kuwa Serikali iko mbioni kufanya maboresho ya sheria mbalimbali ili ziende sambamba na malengo ya Dira Taifa 2050.

Dkt. Homera ametoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano wa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali uliofanyika tarehe 28 Aprili, 2026 Jijini Arusha.

*“Nimpongeze Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameanza vizuri na sasa tunaenda kurekebisha sheria mbalimbali ili ziweze kueandana na malengo ya kufikia Dira ya 2050”.*

Akizungumza katika Mkutano huo, Waziri wa Katiba na Sheria ameeleza kuwa ni muhimu kwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea kujiendeleza kitaalamu na Kimaarifa ili waweze kuishauri vizuri Serikali na kuinua uchumi wa Taifa.

*“Napenda kutoa rai kwenu mzidi kujiendeleza kitaaluma na kimaarifa ili muweze kulishauri vizuri Taifa letu hasa juu ya Sheria zipi zinapaswa kutungwa na kurekebisha kwa ajili ya kuchochea vizuri ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kweli kwa Wananchi wote.”* Amesema Dkt. Homera

Aidha, Dkt. Homera amempongeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Menejimenti ya Ofisi kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

*“Nimshukuru Mhe. Rais kwa kukuteua tena kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali unaitendea haki nafasi hiyo, pia nikupongeze Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali na timu yako kwa maboresho makubwa uliyoyafanya katika Ofisi hii.”* Amesema Mhe. Dkt. Homera. 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari akizungumza awali kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, amesema kuwa ili kufikia malengo ya Dira 2050 ni muhimu kwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakaongeza kasi katika maboresho ya Sheria mbalimbali.

*“Wakati wenzetu wengine wanakuja, wakute tayari tumezifungamanisha sheria zetu na malengo ya Dira 2050 kwa kuzifanya rafiki na wezeshi.

Powered by Blogger.