RAIS SAMIA KUZINDUA MELI KUBWA YA UVUVI WA BAHARI KUU

 


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani anatarajiwa kuzindua Meli ya Kwanza ya Uvuvi wa Bahari Kuu , ambapo uzinduzi wake utafanyika Makao Makuu ya shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO ) Kigamboni Jijini Dar es Salaam.




Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo leo Aprili 17, 2026, wakati wa ziara ya  Kamati ya Uchumi na Uwekezaji ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kutembelea na kukagua ujenzi wa bahari ya uvuvi Kilwa Masoko Mkoani Lindi na kuieleza kamati hiyo kuwa  bandari ya uvuvi Kilwa masoko iliyogharimu shilingi bilioni 280 baada ya kukamilika itafanyiwa majaribio kabla ya kukabidhiwa kwa serikali.


“ Mradi huu kwa sawa  tuko asilimia 97, asilimia tatu zilizobaki ni kwa sababu kuna mitambo mingine imeagizwa ili ifungwe halafu tufanye majaribio kabla ya kukabidhiwa, wakati wowote ndani ya mwezi wa nne na watano mkandarasi anaweza kutukabidhi” alisema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru.

Powered by Blogger.