BINTI PEKEE KITENGO CHA UOKOJI MAGOROFA,MASHIMO MAREFU AONESHA UKAKAMAVU SIKU YA ZIMAMOTO DUNIANI

 


Na Mwandishi wetu--


Dar es salaam


Askari wa Zimamoto na Uokoaji, SGT Leocardia Amiri, ameonyesha ukakamavu wa hali ya juu kama binti pekee anayefanya kazi katika kitengo cha uokoaji kwenye majengo marefu (maghorofa) na mashimo marefu, wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Zimamoto Duniani.



Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ikihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ambaye alishuhudia umahiri na uthubutu wa askari huyo katika utekelezaji wa majukumu yake ya uokoaji.


Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo, “Okoa Maisha na Mali Leo kwa Ajili ya Kesho,” yakilenga kuhamasisha jamii kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto pamoja na kuthamini mchango wa askari wa zimamoto katika kuokoa maisha na mali za wananchi.


Uwepo wa SGT Leocardia katika kitengo hicho nyeti  ambapo Nchi nzima jinsia ya kike wapo wawili anaendelea kuwa chachu ya kuhamasisha wanawake wengi zaidi kujiunga na fani za uokoaji na zimamoto, ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikihusishwa zaidi na wanaume.

Powered by Blogger.